Ticker

6/recent/ticker-posts

Vunjo Wampongeza Dkt. Kimei kwa Uongozi wa Mfano na Miradi ya Maendeleo


Wananchi wa kata mbalimbali katika Jimbo la Vunjo, mkoa wa Kilimanjaro, wamempongeza Mbunge wao Dkt. Charles Kimei kwa utendaji wake bora na uwakilishi wa mfano bungeni,Wamesema tangu alipochaguliwa, amekuwa karibu na wananchi kwa kusikiliza na kushughulikia changamoto zao kwa vitendo.

Baadhi ya miradi iliyotekelezwa chini ya uongozi wake ni pamoja na ujenzi na ukarabati wa barabara, madaraja, vituo vya afya, shule na miradi ya maji, Kata kama Marangu Mashariki, Kahe Mashariki, Makuyuni na Kirua Vunjo Mashariki zimekuwa miongoni mwa zilizofaidika moja kwa moja na miradi hiyo.

Madiwani wa kata mbalimbali pia wamempongeza Dkt. Kimei wakisema siyo tu kuwa ni mbunge kutoka chama chao cha CCM, bali kwa sababu kazi zake zimeonekana kwa macho na zimegusa maisha ya wananchi wengi,Wametaja mafanikio kama uboreshaji wa huduma za afya, elimu, na upatikanaji wa maji safi kama sehemu ya mafanikio ya uongozi wake.

Dkt. Kimei ameendelea kuwasihi wanachama wa CCM kudumisha umoja na kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea wananchi maendeleo kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020–2025.

Post a Comment

0 Comments