NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KAMATI ya Sera ya Fedha ya Benki Kuu ya Tanzania imeamua Riba ya Benki Kuu (CBR) kuendelea kuwa asilimia 6 mara baada kufanya tathmini ya mwenendo wa uchumi, na mwelekeo wake katika robo ya pili ya mwaka 2025.
Kwa muktadha huu, Benki Kuu itaendelea kutekeleza Sera ya fedha ili kuhakikisha riba ya mikopo ya siku saba baina ya benki inabaki ndani ya wigo wa asilimia 4-8.
Ameyasema hayo leo Aprili 4, 2025 Jijini Dar es Salaam, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Yamungu Kayandabila akimwakilisha Gavana wa BoT wakati akitoa taarifa ya kamati hiyo mbele ya waandishi wa habari
Amesema mfumuko wa bei na kasi ya ukuaji wa uchumi nchini, unatarajiwa kubaki ndani ya malengo. Hata hivyo, kutokutabirika kwa sera za biashara na migogoro ya kisiasa duniani inaweza kuathiri mwelekeo wa mfumuko wa bei na ukuaji wa uchumi katika kufikia malengo yake.
"Uamuzi huu wa Kamati unalenga kuukinga uchumi dhidi ya athari zinazoweza kutokea kutokana na vikwazo vya kibiashara na migogoro ya kisiasa duniani". Amesema Dkt. Kayandabila.
Aidha amesema kuwa katika kutathmini mwenendo wa uchumi wa dunia kwa robo ya kwanza ya mwaka 2025, Kamati ilibaini kuwa shughuli za kiuchumi katika nchi zilizoendelea na zile zinazoibukia kiuchumi ziliendelea kuimarika, na mwenendo huu unatarajiwa kuendelea katika robo zijazo za mwaka 2025.
"Mfumuko wa bei ulipungua na kufikia malengo ya benki kuu za nchi nyingi duniani, kutokana na kufifia kwa athari zilizotokana na mitikisiko ya kiuchumi katika vipindi vilivyopita, na utekelezaji wa sera ya fedha iliyolenga kupunguza ongezeko la ukwasi". Ameeleza.
Dkt. Kayandabila amesema kuwa Kutokana na mwenendo huo, pamoja na matarajio ya kuendelea kupungua kwa mfumuko wa bei, benki kuu katika nchi nyingi zimeendelea kupunguza riba zao za Sera ya fedha.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Yamungu Kayandabila akitoa taarifa ya kamati Sera ya Fedha ya Benki Kuu ya Tanzania mbele ya waandishi wa habari leo Aprili 4, 2025 katika ukumbi wa BoT Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wakuu wa Taasisi za fedha wakimfuatilia Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Yamungu Kayandabila akitoa taarifa ya kamati Sera ya Fedha ya Benki Kuu leo Aprili 4, 2025 katika ukumbi wa BoT Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
0 Comments