Ticker

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YAIONGEZEA OSHA WATUMISHI KUIMARISHA UTENDAJI

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Bi. Mary Maganga akihutubia katika Kikao cha Nne cha Baraza la Tano la Wafanyakazi wa OSHA kilichofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kibaha Mkoani Pwani Machi 29, 2025.

*********************

Na Mwandishi Wetu

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeitoa kibali kwa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kuajiri watumishi wapya 74 katika jitihada za kuongeza ufanisi wa Taasisi hiyo kutekeleza jukumu lake la msingi la kulinda nguvukazi ya Taifa.

Mpango huo wa serikali umeelezwa na Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, alipokuwa akimkaribisha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Bi. Mary Maganga kufungua Kikao cha Nne cha Baraza la Tano la Wafanyakazi wa OSHA kilichofanyika mwishoni mwa wiki (Machi 29, 2025) Kibaha Mkoani Pwani.

Kikao hicho kilikuwa na ajenda kubwa moja ambayo ni kujadili mpango wa bajeti wa Taasisi hiyo ya OSHA chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka ujao 2025/2026.

“Tunakushukuru sana Katibu Mkuu wetu kwa kuipigania Taasisi yetu kuongezewa watumishi wengi kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea katika historia ya Taasisi yetu kwani idadi hiyo ya watumishi 74 ni takribani 50% ya watumishi wote wa Taasisi yetu waliopo sasa. Hivyo, tunakupongeza wewe binafsi pamoja na Waziri wetu na tunawaomba mtupelekee salamu zetu kwa Waziri Mkuu na Rais Dkt. Samia kwa kutambua umuhimu wa Taasisi hii na kuendelea kuijengea uwezo,” alieleza Mtendaji Mkuu Bi. Mwenda.

Akiwasilisha hotuba yake ya ufunguzi wa kikao hicho, Katibu Mkuu, Bi.Mary Maganga, ameipongeza Taasisi ya OSHA kwa kuendelea kutekeleza majukumu yake ipasavyo ambapo ameeleza kuwa OSHA ni miongoni mwa Taasisi ambazo Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) inajivunia uwepo wake.

“Niwaombe muendeleze kazi nzuri mnayofanya ya kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya mwaka 2003 pamoja na kanuni zake ambayo serikali yetu iliiweka kwa minajili ya kuhakikisha kwamba rasilimali watu na uwekezaji mwingine vinalindwa,” alieleza Katibu Mkuu katika hotuba yake.

Kwa upande wao Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Bw. Rugemalila Rutatina ambaye ameshiriki kikao hicho, ameipongeza OSHA kwa kuwa mfano bora katika kujenga umoja wa wafanyakazi ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha kufanya maamuzi muhimu ya Taasisi kupitia vikao vya mabaraza ya wafanyakazi kwa mujibu wa sheria za nchi.

Mabazara ya Wafanyakazi nchini yapo kwa mujibu wa Waraka wa Rais Namba 1 wa mwaka 1970 uliowaelekeza waajiri kuwashirikisha wafanyakazi mahali pa kazi katika kupanga, kutekeleza na kutathimini matokeo ya kazi zinazofanyika.
Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, akitoa maelezo ya awali kwenye Kikao cha Nne cha Baraza la Tano la Wafanyakazi wa OSHA kilichofanyika katika Chuo cha Uongozi cha
Mwalimu Nyerere kilichopo Kibaha Mkoani Pwani Machi 29, 2025.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Bi. Mary Maganga (kulia) akibadilishana mawazo na Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda katika Kikao cha Nne cha Baraza la Tano la Wafanyakazi wa OSHA kilichofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kibaha Mkoani Pwani Machi 29, 2025.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Bi. Mary Maganga (katikati) na meza wakiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi na Mameneja wa Vitengo vya OSHA Kikao cha Nne cha Baraza la Tano la Wafanyakazi wa OSHA kilichofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kibaha Mkoani Pwani Machi 29, 2025.
Naibu Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa, Bw. Rugemalila Rutatina akitoa salamu za wafanyakazi
katika Kikao cha Nne cha Baraza la Tano la Wafanyakazi wa OSHA kilichofanyika katika Chuo
cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kibaha Mkoani Pwani Machi 29, 2025.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Bi. Mary Maganga akiwa na meza kuu katika Kikao cha Nne cha Baraza la Tano la Wafanyakazi wa OSHA kilichofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kibaha Mkoani Pwani Machi 29, 2025.
Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na
Naibu Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa, Bw. Rugemalila Rutatina (kulia) katika Kikao cha Nne cha Baraza la Tano la Wafanyakazi wa OSHA kilichofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kibaha Mkoani Pwani Machi 29, 2025.

Wajumbe wa Baraza la OSHA wakifuatilia mawasilisho mbalimbali yaliyowasilishwa katika Kikao cha Nne cha Baraza la Tano la Wafanyakazi wa OSHA kilichofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kibaha Mkoani Pwani Machi 29, 2025.

Post a Comment

0 Comments