Na Mwandishi Wetu.
Dar es Salaam, 28 Machi 2025 - Kampeni ya Magift ya Kugift kutoka YAS na Mixx by YAS imeendelea kubadilisha maisha ya Watanzania, ambapo siku ya tarehe 28 Machi, ilibadili maisha ya ndugu Ramadhani Abdallah Mwinchande, mkazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam baada ya kumkabidhi rasmi gari jipya-zero kilomita, aina ya KIA Sorento. Huyu anakuwa mtanzania wa pili kushinda zawadi hiyo kabambe kupitia promosheni ya YAS ya Magift ya kugift.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi hiyo, Mkurugenzi wa YAS-Kanda ya Dar Kusini, Ndugu Robert Kasulwa, amesema kuwa promosheni hii ni sehemu ya shukrani kwa wateja wa YAS na Mixx by YAS kwa uaminifu wao."Leo tunaandika historia nyingine kwa kumkabidhi mshindi wetu, Ramadhani Abdallah Mwinchande, zawadi ya gari jipya aina ya KIA Sorento. Huu sio tu ushindi wa mtu mmoja, bali ni ushindi wa wateja wetu wote ambao wanaendelea kutumia huduma zetu kila siku. YAS na Mixx by YAS tunaamini kuwa wateja wetu ndio msingi wa kila tunachofanya, na ndio maana tunajitahidi kutoa huduma bora na promosheni zenye thamani halisi," alisema Kasulwa.
Tangu kuzinduliwa kwa kampeni ya Magift ya Kugift, zaidi ya Watanzania 1,300 wamenufaika na zawadi mbalimbali, zikiwemo magari mawili mapya, fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 840, na simu janja zaidi ya 540.Akizungumzia mafanikio ya Kampuni ndani ya siku 100 tangu kufanyika kwa mabadiliko ya chapa kutoka Tigo na Tigopesa kwenda YAS na Mixx by YAS, Kasulwa alibainisha kuwa kampuni hiyo imepokea tuzo mbalimbali, zikiwemo kutoka Ookla, TEHAMA Awards, na TRA kama mlipaji mkubwa wa kodi kupitia ushuru wa forodha.
Mshindi wa gari, Ramadhani Abdallah Mwinchande, alishukuru YAS na Mixx by YAS kwa zawadi hiyo na kusisitiza kuwa ushindi wake ni uthibitisho kuwa kila mteja ana nafasi ya kushinda kupitia promosheni hii."Nina furaha kubwa kupokea zawadi hii. Nilipopigiwa simu kuambiwa nimeshinda gari, mara ya kwanza sikuamini. Lakini YAS walinihakikishia ushindi wangu na kweli leo naondoka na gari jipya. Nawashukuru YAS na Mixx by YAS kwa kutambua na kuthamini wateja wake," alisema Mwinchande.
Kwa upande wake, Kasulwa aliwahimiza wateja kuendelea kushiriki katika promosheni mbalimbali zinazoendelea na kutumia huduma za YAS na Mixx by YAS, akisisitiza kuwa kampuni hiyo itaendelea kuwa karibu na wateja wake kwa kutoa huduma bora na kuwapa fursa zaidi za kushinda.
0 Comments