Na Mwandishi Wetu.
Mtandao namba moja nchini kwa utoaji wa Huduma za Kidigitali Yas Tanzania , kupitia Kampeni yake ya MAGIFTI YA KUGIFTI umeendelea kukonga mioyo ya wateja wake kwa kuwazawadia zawadi mbalimbali za Fedha Taslimu Milioni 1 - 5 , Simu Janja na Zawadi za Magari Mapya kabisa , ambapo hadi sasa wiki ya 10 Mtandao huo umeshatoa zawadi za Fedha zaidi ya Milioni 250 , unachotakiwa kufanya ili kuibuka mshindi wa zawadi hizo ni kununua Vifurushi kupitia MIXX BY YAS ( zamani Tigo Pesa ) , kufanya miamala , malipo ya Kiserikali n.k ndo siri pekee ya ushindi .
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa baadhi ya Washindi wa Wiki hii ya 10 Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Yas - Bi. Mwangaza Matotola amewasihi wateja , na watanzania kwa ujumla kufanya miamala ya Mixx by Yas kwa wingi ndani ya Wiki hizi mbili zilizobaki ili kujishindia simu , Fedha na Zawadi kubwa ya Gari.
0 Comments