Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi akiwasilisha taarifa ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali mbele ya Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kilichofanyika Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya kudumu Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akiendesha kikao cha kamati hiyo na Viongozi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali na Wizara ya Katiba na Sheria kilichofanyika Jijini Dodoma. Kushoto ni Katibu wa Kamati hiyo Ndugu Ganjatuni Kilemile.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala, Katiba na Sheria na Viongozi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali (hawapo pichani) wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichofanyika Jijini Dodoma.
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bi. Alice Mtulo akifuatilia wasilisho la Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Ally Possi (hayupo pichani) kuhusu majukumu ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati wa kikao cha Kamati ya kudumu ya Bunge Utawala, Katiba na Sheria na Ofisi hiyo kilichofanyika Jijini Dodoma.
Wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakifuatilia wasilisho la Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi (hayupo pichani) kuhusu majukumu ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati kikao kilichofanyika Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakifuatilia wasilisho la Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi (hayupo pichani) kuhusu majukumu ya Ofisi hiyo wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kilichofanyika Jijini Dodoma.
0 Comments