Kampuni ya Yas Tanzania imekuwa ikiendesha kampeni hiyo, kwa muda wa wiki 12 ambapo mpaka sasa zaidi ya kiasi cha shilingi mil. 300, zimeshatolewa kwa washindi mbalimbali miongoni mwa zawadi hizo pesa taslimu na simu za mkononi.
Kwa upande wake mmoja wa washindi wa milioni moja wa wiki hii Herieth Charles Maimu, ameishukuru Yas kwa kuendesha kampeni hiyo kwani imekuwa ikisaidia kuwapatia zawadi mbalimbali wateja wake ikiwemo pesa taslimu na zawadi nyinginezo.Naye Bi. Prescious Stanlaus Mallya, amesema yeye ameibuka mshindi na hatimaye kipigiwa simu baada ya kufanya miamala mara kwa mara jambo lililopelekea kuibuka mshindi hivyo amewataka Watanzania wengine kutumia mtandao wa Yas Tanzania kwani ni mtandao wenye huduma bora.
Yas ikishirikiana na Kitengo cha Mixx by Yas imekuwa ikiendesha kampeni ya Magift ya Kugift ambapo wateja na washiriki wamekiri kuwa ni ya ukweli na uwazi na kuwa kila mtu anaweza kushida.
Kwa upande wake Meneja wa Wateja Maalum wa Mixx by Yas, Mary Rutta amewapongeza washindi wote waliokwenda kuchukua zawadi zao katika droo hiyo ya 11 ambapo ametumia hafla hiyo kuwataka wateja wengine wa Mixx by Yas pamoja na Yas Tanzania kuendelea kushiriki kampeni hiyo kwa kutumia huduma za Yas.
Aidha Rutta amesema wao kama Yas wanatambua ugumu unaopatikana kwenye mwezi huu wa Januari kwa Watanzania hususani wazazi hivyo kampuni Yao imekuwa ikiwezesha kwa kuwapa fedha na zawadi mbalimbali ilikuwakwamua katika kipindi hiki.
Kampuni ya Mawasiliano ya Yas inaendesha kampeni hiyo, ambapo mshindi wa jumla anatarajiwa kuondoka na zawadi ya gari aina ya Kia Sorante 0.KM wakati mshindi mwingine ataondoka na Shilingi mil 50. katika droo mwisho.
0 Comments