Ticker

6/recent/ticker-posts

TBS NA ZBS WAWAFIKIA WANANCHI NA WAJASIRIAMALI MAONESHO YA 11 YA BIASHARA ZANZIBAR

                                




Maafisa kutoka Shirika la Viwango Tanzania ( TBS ) na Shirika la Viwango Zanzibar ( ZBS ) wakitoa elimu kwa wajasiriamali kuhusu umuhimu wa kuwa na alama ya Ubora katika bidhaa zao, ni katika Maonesho ya 11 ya Kimataifa ya Biashara visiwani Zanzibar yanayoendelea katika viwanja vya Fumba Dimani kuanzia tarehe 1 Januari 2025 na yanatarajiwa kumalizika tarehe 15 Januari,  ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Na Mwandishi Wetu.

Shirika la Viwango Tanzania ( TBS ) na Shirika la Viwango Zanzibar ( ZBS ) wametoa elimu kwa wajasiriamali kuhusu umuhimu wa kuwa na alama ya Ubora katika bidhaa zao katika Maonesho ya 11 ya Kimataifa ya Biashara visiwani Zanzibar yanayoendelea katika viwanja vya Fumba Dimani kuanzia tarehe 1 Januari 2025 na yanatarajiwa kumalizika tarehe 15 Januari.

Akizungumza katika Maonesho hayo Afisa Uhusiano na Masoko TBS Bi. Maryam Abdulaziz amesema kama ilivyo kawaida siku zote moja ya majukumu ya Shirika ni kutoa elimu ya Viwango kwa wananchi na umuhimu wa kuzingatia viwango kwa wajasiriamali na wafanya biashara mbalimbali , ivyo basi Shirika limetumia maonesho hayo , kuwafikia wananchi , wafanya biashara na Wajasiriamali wanaoishi na kufanya shughuli zao Visiwani Zanzibar.

Tumewahimiza wafanya biashara na wajasiriamali wa hapa Visiwani Zanzibar  kujitokeza kwa wingi kwenye ofisi za Shirika la Viwango Zanzibar  (ZBS) kwa ajili ya kuthibitisha ubora wa bidhaa wanazozalisha ili kuondokana na vikwazo vya kibiashara ndani na nje ya nchi, habari njema ni kwamba kwa wajasiriamali gharama za kupata alama za ubora ni bure, kwani tayari zinalipwa na Serikali " amesema Bi. Maryam

Post a Comment

0 Comments