Ticker

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YATENGA BILIONI 14.48 MRADI WA ENGARUKA


WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo Januari 10,2025 katika Kata ya Engaruka wilayani Monduli.

Na.Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo,amesema Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 14.48 kwa ajili ya ulipaji wa fidia katika mradi wa magadi soda wa Engaruka ambapo shilingi billion 6.2 zitatumika katika ulipaji fidia kwa wananchi waliopisha mradi huo.

Waziri Jafo,ameyasema hayo leo Januari 10,2025 wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Engaruka wilayani Monduli.

Amesema kuwa wananchi 595 kutoka vijiji vinne vya Engaruka Chini, Mbaash, Idonyonado na Irerendeni watanufaika na fidia hiyo ya shilingi bilioni 6.2 huku fedha zingine zilizobaki zikienda katika shughuli mbalimbali za miradi mbalimbali ya huduma za kijamii.

Katika mkutano huo, Dkt. Jafo amewapa habari njema wananchi wa Kata hiyo ya Engaruka kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan tayari ameshatoa pesa za kuwalipa fidia wananchi hao watakaopisha mradi.

"Mradi huo tayari umetangazwa kwa lengo la kutafuta wawekezaji ambapo hadi sasa Makampuni kadhaa tayari wameonyesha nia ya kuwekeza kwenye mradi huu".amesema Dkt.Jafo

Aidha Dkt. Jafo amesema fedha hizo zimetolewa na Serikali ikiwa ni mkakati wa kuendeleza miradi ya kimkakati yenye tija kwa Taifa.

Dkt. Jafo mradi huo ni muhimu sana kwa uchumi wa Taifa kwani Viwanda vingi nchini vinatumia magadi soda kama malighafi muhimu vikiwemo viwanda vya kutengeneza vioo, sabuni, nguo, nk.

Aidha, Dkt. Jafo amesema kwamba mradi huo utasaidia sana kuokoa matumizi ya fedha za kigeni ambazo kwasasa zinatumia kuagiza Magadi soda kutoka nje ya nchi.

Katika kuweka msisitozo, Jafo amewashauri wananchi hao kuanza kufikiria kujenga hotel na nyumba za kulala Wageni na kubuni biashara mbalimbali za huduma kwani eneo hilo litafikiwa na wageni wengi wanaokuja kufanya kazi katika viwanda vitakavyojengwa eneo hilo.


Naye Naibu Waziri wa Madini, Mhe.Dkt.Stephen Kiruswa amesema mradi huo uwe ni chimbuko la mafanikio kwa wananchi wa wilaya ya Monduli na Longido kwani mradi huu ni mkubwa na unatija Kwa wananchi.
 

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo Januari 10,2025 katika Kata ya Engaruka wilayani Monduli.

Post a Comment

0 Comments