Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Dodoma
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amesema wananchi hawana mashaka kuhusu CCM kwani ni Chama kikubwa kuliko chama chochote nchini kimuundo, idadi ya wanachama, historia,wingi wa wanachama na oganaizesheni.
Pia amesema CCM kitaendelea kufanya mageuzi makubwa ya kimfumo, utendaji na uendeshaji hivyo wanachama na viongozi wanapaswa kutimiza wajibu wao kwa kuzingatia uzalendo na kuacha kufanyakazi kwa mazoea.
Akizungumza mbele ya maelfu ya wanachama wa Chama Cha Mqpinduzi wakati Mkutano Mkuu maalum , Dk.Samia amesisitiza kuwa CCM ni chama kikubwa,hivyo hakuna sababu ya kuwa na shaka nacho.
Ametoa mwito kwa wajumbe wa mkutano huo kuhakikisha wanaendelea kuhamaisha wananchi kujiandikisha au kurekebisha taarifa zao katika daftari la kudumu la wapigakura na kusikiliza kisha kutatua kero za wananchi.
Akizungumza kuhusu kuimarika kwa Chama hicho Rais Samia amesema kimeendelea kuimarika na kwamba hadi kufikia Desemba mwaka 2024 idadi ya wanachama wake wamefikia milioni 12,104,823 kutoka wanachama milioni tatu.
Amesema Chama kimefanya oparesheni maalum na watu walikuwa wakisubiri kujiandikisha katika Chama chao hivyo amezipongeza jumuiya zote za Chama kwa kufanya kazi kubwa iliyowezesha kuwa na idadi kubwa ya wanachama.
Akizungumzia utekelezaji shughuli za chama kuanzia mwaka 2022 hadi mwaka 2024 lakini na taarifa ya utekelezaji Ilani ya Uchaguzi ya CCM kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) amesema Mkutano Mkuu wa CCM uliopita maazimio mbalimbali yalifikiwa ikiwemo kuiagiza serikali kuchukua hatua za kiutendaji katika kuimarisha utendaji wa Chama na serikali.
Ametaja maagizimio mengine ni kutoa mafunzo kuhusu falsafa ya ujamaa na kujitegemea katika mazingira ya sasa, kuendeleza mageuzi ya kiuchumi kwa kuzingatia sera, demokrasi pamoja na kuimarisha matumizi ya tehama katika utendaji wa shughuli za Chama.
Dk.Samia amesema katika kutekeleza azimio hilo, CCM kimeendesha mafunzo ya kiutendaji nje na ndani ya nchi na kufafanua kwa upande wa nje ya nchi mafunzo yalitolewa zaidi katika nchi za China na India.
"Tumerahisisha shughuli za kiutendaji wa Chama na jumuiya zake kwa kununua vyombo vya usafiri kuanzia kwenye mashina hadi mikoa. magari 194 yamesambazwa katika ofisi 149 za wilaya, magari 33 ofisi za CCM mikoa yote, magari tisa ambapo matatu kila jumuiya za CCM.
"Shabaha yetu kuhakikisha wilaya ziliobaki zinapata magari mapya kabla ya uchaguzi mkuu. Katika ngazi ya kata na wadi za CCM, tumegawa pikipiki nne kwa kila ofisi ambapo hadi Novemba mwaka jana zoezi hilo limefanyika kwa asilimia 100," alieleza.
0 Comments