Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AWAONYA WANAOJIPITISHA MAJIMBO NA KUANZA KUFANYA KAMPENI KABLA YA WAKATI

Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Dodoma

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan amewaonya wanachama wa CCM wenye nia ya kugombea nafasi za udiwani na Ubunge katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2025 ambao wameanza kupita pita majimboni na katika kuanza kufanya kampeni kabla ya wakati.

Dk.Samia ametoa onyo hilo leo Januari 18,2025 jijini Dodoma ambako kunafanyika Mkutano Mkuu maalum kwa ajili ya kujaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho pamoja na kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani kuanzia mwaka 2020 hadi mwaka 2024ubunge na udiwani ambao wameanza kampeni za mapema kabla ya wakati.

Akieleza kuhusu walioanza kampni kabla ya wakati Dk.Samia amesema kwamba Chama kimepata ushahidi ambao unaonesha wapo baadhi ya watu wakiwakusanya wananchi kwa madai ya kuwawezesha kupitia shughuli za kijamii lakini lengo ni kutaka kujitambulisha kwa wapiga kura.

“Wanachama wenye tabia ya kuendeleza makundi katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu badala ya kuwaunga mkono wagombea waliopitishwa na Chama.Kwa wale ambao wamejipanga kugombea wasubirie wakati ufike.

“Tunakemea kampenzi ambazo zinaanza mapema kabla ya wakati .Tumeshapokea malalamiko na ushahidi wa picha za watu wanaofanya misafara kwenda majimboni, wanaitisha mikutano ya jimbo kwa kigezo cha ufungaji ila malengo yao ni kujitambulisha kwa wanachana.Nawaonya wote wenye tabia hii kuacha mara moja”natoa onyo," Rais Dk. Samia alikemea.

Kuhusu makundi ,Rais Samia ametumia nafasi hiyo ya Mkutano Mkuu maalum amekemea baadhi ya wanachama wenye tabia ya kuendeleza makundi katika uchaguzi mkuu huku akifafanua kuna baadhi ya wanaCCM wamekuwa wakiendeleza makundi ya uchaguzi licha ya Chama kupitisha jina la mgombea.

“Tunaposema makundi ndani ya Chama wakati wa kuomba ni kwa sababu ya demokrasia na tunafahamu waombaji wanakuwa wengi hivyo tutqpata makundi lakini tutakaposimamisha wagombea wa Chama chetu tunaomba makundi yasiendelee," amesema Rais Samia alipokuwa alipokuwa anakemea makundi.

Pia amesema katika mwaka huu wa uchaguzi, wanachama wanawajibika kuendelea kuwa wamoja zaidi katika kukamilisha ushindi wa CCM kwani maendeleo ya nchi yapo mikononi mwa CCM huku akitoa rai ya wana CCM kutodharu vyama vya upinzani au kuingia uwoga dhidi ya vyama hivyo.


Post a Comment

0 Comments