Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa (katikati) akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi Milioni 25 kwa mwakilishi wa Association for the Termination of Female Genital Matilation(kushoto). Fedha hizo zimetolewa na Taasisi ya kimataifa ya Nos Vies en Partage (NVeP) kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick
Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa (katikati) akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi Milioni 25 kwa mwakilishi wa shirika la Fageme Group (kushoto). Fedha hizo zimetolewa na Taasisi ya kimataifa ya Nos Vies en Partage (NVeP) kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick
****
Taasisi ya kimataifa ya Nos Vies en Partage (NVeP), kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick, imetoa msaada wa shilingi milioni 100 kwa mashirika manne yasiyo ya kiserikali kwa ajili ya kukabilianana changamoto mbalimbali.
Mashirika yaliyonufaika na msaada huo kila moja likiwa limepata shilingi milioni 25 ni Youth Wellbeing Initiative, Fageme Group, Association for the Termination of Female Genital Matilation na Bulyanhulu Agriculture Group.
Msaada huo umetokana na sehemu ya fedha zilizotolewa na taasisi ya Nos Vies en Partage (NVeP), iliyoanzishwa na inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow, kwa ajili ya kusaidia makundi maalum kama vile Wanawake, watoto na makundi mengine yenye uhitaji yasiofaidika na ukuaji wa kiuchumi barani Afrika.
Kila robo ya mwaka taasisi ya NVeP, imeweza kutoa misaada yenye tija na manufaa ya moja kwa moja kwenye jamii mbalimbali zenye uhitaji barani Afrika na kufikia sasa zaidi ya mashirika 30 yasiyo ya Kiserikali na taasisi za kijamii nchini yamepatiwa msaada huo na tayari umeleta mabadiliko chanya katika jamii hususani katika sekta ya elimu, afya kwa Wanawake na watoto na utunzaji wa Mazingira.
Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wakati wa ziara yake ya kikazi nchini, Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow, amesema kuwa taasisi ya ya NVeP, itaendelea kusaidia mashirika yasiyo ya kiserikali na taasisi ambazo zinatoa huduma kwa jamii kuendana na malengo ya taasisi hiyo sambamba na kuleta mabadiliko chanya katika jamii na kuwataka wanufaika kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa
Akiongea kwa niaba ya wanufaika wenzake, Meneja wa shirika la na Association for the termination of Female Genital Matilation lenye makao yake wilayani Tarime mkoani Mara,Valerian Mgani, ameshukuru NveP kwa msaada huo na kueleza kuwa utasaidia kukabiliana na changamoto za kijamii kupitia taasisi hizo.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow (kulia) akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa shilingi milioni 100 kwa mashirika manne yasiyo ya kiserikali kwa ajili ya kukabilianana changamoto mbalimbali zilizotolewa na Taasisi ya kimataifa ya Nos Vies en Partage (NVeP), kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick.
Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa (katikati) akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi Milioni 25 kwa mwakilishi wa shirika la Youth Wellbeing Initiative (kushoto). Fedha hizo zimetolewa na Taasisi ya kimataifa ya Nos Vies en Partage (NVeP) kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick
Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa (katikati) akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi Milioni 25 kwa mwakilishi wa Association for the Termination of Female Genital Matilation(kushoto). Fedha hizo zimetolewa na Taasisi ya kimataifa ya Nos Vies en Partage (NVeP) kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick
Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa (katikati) akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi Milioni 25 kwa mwakilishi wa Bulyanhulu Agriculture Group (kushoto). Fedha hizo zimetolewa na Taasisi ya kimataifa ya Nos Vies en Partage (NVeP) kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick
Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa (katikati) akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi Milioni 25 kwa mwakilishi wa shirika la Fageme Group (kushoto). Fedha hizo zimetolewa na Taasisi ya kimataifa ya Nos Vies en Partage (NVeP) kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick
0 Comments