Na Oscar Assenga,Tanga
MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa tena kiasi cha shilingi bilioni 4.7 ili mkandarasi wa kampuni ya Chiko anayejega barabara ya Tanga hadi Pangani kwa kiwango cha lami aendelee na kazi baada ya kusimama muda mrefu.
Ummy aliyasema hayo leo wakati wa ziara ya Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega wakati alipotembelea ujenzi wa barabara ya Tanga-Pangani na kuwahakikishia wananchi waliojitokeza eneo la Kirare kunakojengwa daraja kwamba serikali imetoa fedha hizo ili ujenzi wa barabara hiyo uendelee.
Mbunge aliishukuru serikali kwa kueleza kwamba anamshukuru Rais Dkt Samia kwa kutoa fedha hizo ambazo zitasaidia kuendelee kwa kazi za ujenzi kwa mkandarasi huyo ambaye alismama akisubiri malipo yake ya awamu ya pili.
“Mheshimiwa Waziri tufikishie salamu zetu kwa Rais, tunamshukuru sana kwa kutoa fedha hizi ambazo zitamfanya mkandarasi kurejea kazini na kazi ya ujenzi wa barabara hii utaendelea,” alisema Ummy ambaye amekuwa kipenzi cha wana Tanga.
Ummy alisema kukamilika kwa barabara ya Tanga Pangani kutainua uchumi wa wilaya hizo na manufaa yake ni makubwa na wanaamini ujio wa Waziri Ulega hauwezi kumuagusha Rais hiyo ujenzi huo utaenda kwa kasi ili waweze kufaidi matunda ya barabara ya Tanga-Pangani.
“Lakini hili daraja kwetu ni maafuru lilikuwa kero sana na barabara ikiishia Tanga Panga tutakuwa tunatumia dakika 30 hadi 25 kutoka Tanga hadi Pangani hivyo tufikishe salamu shukrani kwa Rais kwa kuwekeza fedha nyingi hapa kwani itainua uchumi na kufungua Tanga ikashindane na Mombasa Kenya”Alisema
Hata hivyo alisema kwamba barabara hiyo ni ya kimkakati na inagusa kata 8 kati ya kata 27 za Tanga mjini huku akieleza kati ya hizo moja ambayo ni ya Kirare imekuwa ikilima zao la Muhogo na hivyo kusafirishwa kwenda sokono hivyo ujenzi utakapokamilika utaweza kuufungua mkoa wa Tanga na RC Dkt ,Balozi Batilda Burian amekuwa akipigania suala la kuinua utalii Tanga na ukienda Mombasa unaona nyari kumechangamka.
Mbunge Ummy alisema hivyo barabara hiyo ni muhimu kwani Tanga wana beach nzuri lakini kutokana na kutokuwa na barabara nzuri watu wanashindwa kwenda kufurahia uwepo wake .
Akizungumza katika eneo hilo Waziri Ulega aliiomba kampuni ya Chiko inayojenga barabara hiyo kurudi na kurejesha mitambo yao ili waweze kuendelea na kazi ya ujenzi wa barabara hiyo ya kilomita 50.
Alisema Rais alisikia kilio cha mbunge wa Tanga pamoja na mbunge wa Pangani Jumaa Aweso ambao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakiiomba serikali itoe fedha za ujenzi wa barabara hiyo.
“Rais amesikia kilio cha wabunge wenu wa Tanga na Pangani na mkandarasi tunakuomba rudi site uendelee na ujenzi na fedha nyngine utaendelea kulipwa ili baraara hii ikamilike wananchi wa Tanga wana kiu kubwa ya kuitumia barabara hii ili iwanufaishe kiuchumi” alisema
0 Comments