Ticker

6/recent/ticker-posts

MALIASILI, MAMBO YA NDANI ZATAKIWA KUSHIRIKIANA KUKUZA UTALII

Na Happiness Shayo-Dodoma

Wizara ya Maliasili na Utalii imetakiwa kushirikiana kwa ukaribu na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kukuza soko la utalii nchini na kurahisisha utoaji wa huduma ya viza kwa watalii.

Hayo yamesemwa leo Januari 14,2025 na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhe. Timotheo Mnzava katika kikao kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma.

“Wizara ya Mambo ya Ndani, Uhamiaji na Wizara ya Maliasili na Utalii mshirikiane kuikuza Sekta ya Utalii, tunahitaji mfanye zaidi kuisaidia sekta hii na kama kuna changamoto mkazitatue” Mhe. Mnzava amesisitiza.

Mhe. Mnzava amezitaka Wizara hizo kuoanisha mifumo ya malipo kwa watalii na kuweka mikakati madhubuti ya kutambua masoko muhimu ya watalii na kuwavuta waje nchini sambamba na kurahisisha michakato ya kupata viza kwa watalii hao.

Naye, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) ameiahidi kamati hiyo kwamba Wizara ya Maliasili na Utalii itahakikisha inafanya kazi kwa ukaribu na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuhakikisha soko la utalii linakua ili kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kukuza Sekta ya Utalii nchini.

Tutahakikisha tunatambua masoko muhimu ya utalii na kuweka mikakati madhubuti ya kuvutia watalii kwa kushirikiana ”Mhe. Chana amesema.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Viongozi na Watendaji mbalimbali kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zake pamoja na Viongozi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ndani ya Nchi na Uhamiaji.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhe. Timotheo Mnzava(Mb) akitoa maelekezo kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu namna bora ya kuiboresha Sekta ya Utalii kwa kurahisisha upatikanaji wa viza kwa watalii, katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kilichofanyika leo Januari 14,2025 Bungeni jijini Dodoma.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) akizungumza katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii  kilichofanyika leo Januari 14,2025 Bungeni jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi , Mhe. Daniel Sillo (Mb) akiwasilisha Taarifa ya Serikali kuhusu hali ya upatikanaji wa Viza kwa Watalii wanaoingia nchini kutoka mataifa mengine, katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii  kilichofanyika leo Januari 14,2025 Bungeni jijini Dodoma.

Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi (kulia) na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Nkoba Mabula (kushoto) wakifuatilia wasilisho la  Taarifa ya Serikali kuhusu hali ya upatikanaji wa Viza kwa Watalii wanaoingia nchini kutoka mataifa mengine, ikiwasilishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi , Mhe. Daniel Sillo (Mb)(hayupo pichani) katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii  kilichofanyika leo Januari 14,2025 Bungeni jijini Dodoma.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) akizungumza katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii  kilichofanyika leo Januari 14,2025 Bungeni jijini Dodoma.

Post a Comment

0 Comments