Na Mwandishi Wetu.
Hatimaye Kampuni ya Mawasiliano ya Yas Tanzania jana Januari 7, 2025 imekabidhi zawadi ya Tsh Mil 10 kwa Athumani Mrisho Kutoka mkoani Tanga, mshindi wa Droo ya 8 ya promosheni ya "MAGIFTI YA KUGIFTI”
Kwa upande wake Meneja Mauzo wa Yas Mkoa wa Tanga Amani Sailoja amempongeza, mshindi , huyo Kutoka Wilayani Mkinga, ambapo mbali na mambo mengine amesema ametumia hafla hiyo kuwataka wateja wengine WA Mixx by Yas pamoja na Yas Tanzania kuendelea kushiriki Promoshe hiyo kwani kila mmoja ana fursa ya kujishinda zawadi hizo.
Meneja mauzo wilaya ya Muheza Telly Maile, pamoja na. Meneja wa Biashara na masoko wa kampuni hiyo Pwani ya kaskazini mkoani humo Mohamed Bagasha kwa pamoja wametumia hafla hiyo, kuwashukuru wateja WA Yas kwa kuendelea kutumia mtandao huo,ikiwemo kufanya miamala ya mara kwa mara na hatimaye kujishindia zawadi Kutoka Magift ya Kugift.
Kampuni ya YAS Tanzania imekuwa Ikiendesha promosheni hiyo, kwa muda WA wiki 12 ambapo hadi kufikia Leo zaidi ya kiasi cha Shilingi Zaidi ya mil. 250 zimeshatolewa zikienda kwa washindi mbalimbali sambamba na zawadi hizo zikiwemo simu za mkononi
0 Comments