Na Benny Mwaipaja, Dodoma
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amesema kuwa Tanzania ina thamini mchango mkubwa wa Taifa la Marekani katika maendeleo ya nchi kupitia miradi na program mbalimbali zinazofadhiliwa na nchi hiyo, ukiwemo Mkataba wa Msaada wa dola za Marekani bilioni 1.14, uliosainiwa hivi karibuni kwa ajili kuendeleza sekta mbalimbali.
Dkt. Nchemba, ameyasema hayo Jijini Dodoma, wakati akiagana na Balozi wa Marekani aliyemaliza muda wake wa uwakilishi nchini Tanzania, Mhe. Michael Battle, ambapo walitumia fursa ya kikao hicho kujadili maeneo mapya ya ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani hususan katika sekta za biashara na uwekezaji.
“Ninashukuru kwa msaada wa dola za Marekani bilioni 1.14 uliotolewa na Taasisi za Marekani kupitia Program ya Development Objectives Agreement (DOAG), unaoonesha namna Marekani inavyochangia maendeleo ya nchi yetu, ambapo fedha hizo zitaelekezwa kwenye sekta za afya, elimu, kukuza uchumi na utawala bora, hivyo kuchangia Agenda ya Dira ya Taifa ya 2025 na Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2021/22–2025/26. ” alisema Dkt. Nchemba.
Mhe. Dkt. Nchemba alirejea pia shukrani zake kwa Marekani kwa kuipa nafasi Tanzania ya kuboresha masuala kadhaa kupitia Mradi wa Millenium Challenge Corporation (MCC), ili nchi iweze kurejea kwenye mpango mkuu wa maendeleo na kwamba Serikali ya Awamu ya Sita imeimarisha kwa kiasi kikubwa misingi ya demokrasia, haki za binadamu, utawala bora pamoja na maendeleo ya nchi.
Kwa upande wake, Balozi wa Marekani aliyemaliza kipindi chake hapa nchini, Mhe. Michael Battle, alieleza kuwa Marekani na Tanzania ni washirika wa muda mrefu wa maendeleo na kwamba uhusiano huo umeendelea kudumishwa na kuimarishwa hadi sasa.
Mhe. Balozi Battle, aliyeambatana na Naibu wake Bw. Andrew Lentz, alisema kuwa ushirikiano huo unatarajia kuchukua mwelekeo mpya kwa kuhimiza zaidi biashara na uwekezaji kwa faida ya pande zote mbili hususan kwa kutumia ukanda wa kibiashara wa Bahari ya Hindi pamoja na uwepo wa fursa ya gesi (LNG)..
Aidha, alisema kuwa Marekani inaandaa mpango mpya wa kutumia Sheria ya ukuaji wa fursa Afrika (AGOA) unaolenga kukuza masoko na biashara ndani na nje ya Marekani, ambapo mwelekeo utakuwa ni ushirikiano wa kibishara kati ya nchi na nchi (bilateral) badala ya Marekani na Mataifa mengi kwa pamoja (Multilateral).
Mazungumzo ya kuagana na Balozi wa Marekani aliyemaliza muda wake nchini Tanzania, Mhe. Michael Battle, yalimhusisha pia Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamisi Shaaban, Viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha, na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (Kulia), akiagana na Balozi wa Marekani nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mhe. Michael Battle, baada ya kikao chao jijini Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine, Mhe. Dkt. Nchemba alimshukuru kwa ushirikiano mzuri katika kipindi chote cha uongozi wake kwa kufanyakazi kwa karibu na Serikali katika miradi ya maendeleo nchini na kumwomba aendelee kuwa Balozi mzuri wa Tanzania hata baada ya kumaliza kipindi chake cha utumishi nchini Tanzania.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (Katikati) akizungumza jambo wakati wa kikao chake na Balozi wa Marekani nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mhe. Michael Battle (hayupo pichani), baada ya kikao chao jijini Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine, Mhe. Dkt. Nchemba alimshukuru kwa ushirikiano mzuri katika kipindi chote cha uongozi wake kwa kufanyakazi kwa karibu na Serikali katika miradi ya maendeleo nchini na kumwomba aendelee kuwa Balozi mzuri wa Tanzania hata baada ya kumaliza kipindi chake cha utumishi nchini Tanzania.
Balozi wa Marekani nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mhe. Michael Battle (Katikati), akizungumza jambo wakati wa kikao chake na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (hayupo pichani), wakati wa kikao chao kilichofanyika jijini Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine, Mhe. Dkt. Nchemba alimshukuru kwa ushirikiano mzuri katika kipindi chote cha uongozi wake kwa kufanyakazi kwa karibu na Serikali katika miradi ya maendeleo nchini na kumwomba aendelee kuwa Balozi mzuri wa Tanzania hata baada ya kumaliza kipindi chake cha utumishi nchini Tanzania.. Kulia ni Naibu Balozi wa Marekani nchini, Bw. Andrew Lentz.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (wa tatu kulia) akimsikiliza Balozi wa Marekani nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mhe. Michael Battle (hayupo pichani) wakati wa kikao chake na Balozi huyo, kilichofanyika jijini Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine, Mhe. Dkt. Nchemba alimshukuru kwa ushirikiano mzuri katika kipindi chote cha uongozi wake kwa kufanyakazi kwa karibu na Serikali katika miradi ya maendeleo nchini na kumwomba aendelee kuwa Balozi mzuri wa Tanzania hata baada ya kumaliza kipindi chake cha utumishi nchini Tanzania. Wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamisi Shaaban (wa tatu kushoto), Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Patrick Pima (wa pili kushoto), na Maafisa wengine wandamizi wa Wizara ya Fedha.
Balozi wa Marekani nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mhe. Michael Battle (Katikati), akizungumza jambo wakati wa kikao chake na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (hayupo pichani), wakati wa kikao chao kilichofanyika jijini Dodoma, ambapo ameahidi kuendelea kuwa Balozi mzuri wa Tanzania popote atakapokuwa hususan katika kuvutia fursa lukuki za biashara na uwekezaji zinazopatikana nchini Tanzania.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (Kulia), akimkabidhi zawadi ya baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya hapa nchini, Balozi wa Marekani nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mhe. Michael Battle, baada ya kikao chao jijini Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine, Mhe. Dkt. Nchemba alimshukuru kwa ushirikiano mzuri katika kipindi chote cha uongozi wake kwa kufanyakazi kwa karibu na Serikali katika miradi ya maendeleo nchini na kumwomba aendelee kuwa Balozi mzuri wa Tanzania hata baada ya kumaliza kipindi chake cha utumishi nchini Tanzania.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (Katikati), Balozi wa Marekani nchini Tanzania aliyemaliza muda wake, Mhe. Michael Battle (wa nne kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Balozi wa Marekani nchini, Bw. Andrew Lentz (wa tatu kushoto), Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamisi Shaaban (wa nne kulia), Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Patrick Pima (wa pili kushoto), Kaimu Mratibu wa Program za Millenium Challenge Corporation-Tanzania (MCC), Dkt. Muhajir Kachwamba (wa tatu kulia) na Maafisa wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, baada ya kumalizika kwa kikao chao, jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)
0 Comments