Na Mwandishi Wetu.
Mtandao namba moja nchini kwa utoaji wa Huduma za Kidigitali wa Yas Tanzania, leo hii Januari 10, 2025, imekabidhi zawadi kwa washindi wa wa kampeni ya “Magift Kugift hii ikiwa ni droo ya 9.
YAS Tanzania imekuwa itaendesha promosheni hiyo, kwa muda wa wiki 12 ambapo hadi kufikia leo zaidi ya kiasi cha shilingi za Kitanzania zaidi ya mil. 260 zimeshatolewa zikienda kwa washindi mbalimbali sambamba na zawadi hizo zikiwemo simu za mkononi na zawadi kubwa ya gari jipya.
Naye Bi. Rehema Maarifa Salum ambaye ni mjasiriamali wa kuuza samaki Chamazi Mbande Dar, amesema yeye ameibuka mshindi na hatimaye kupigiwa simu baada ya kufanya miamala mara kwa mara jambo lililopelekea kuibuka mshindi hivyo amewataka Watanzania wengine kutumia mtandao wa Yas kwani ndiyo mtandao unaoongoza kwa huduma bora na pia Yas ikishirikiana na Kitengo cha Mixx by Yas imekuwa ikiendesha kampeni ya Magift ya Kugift ambapo wateja na washiriki wamekiri kuwa ni ya ukweli na uwazi na kuwa kila mtu anaweza kushida.
Kwa upande wake Meneja wa Wateja Maalum kutoka Mixx by Yas, Mary Rutta amewapongeza washindi washindi waliopatikana wiki hii ya tisa ambapo ametumia hafla hiyo kuwataka watumiaji wengine wa simu kutumia mtandao wa Yas na kufanya miamala kwa Mixx by Yas ili kushiriki kampeni hiyo kwani kila mmoja ana fursa ya kujishinda zawadi hizo.
0 Comments