Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI KOMBO ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO UBALOZI WA INDIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amesaini Kitabu cha Maombolezo Ubalozi wa India nchini kufuatia kifo cha Waziri Mkuu Msataafu wa India, Mhe. Manmohan Singh, kilichotokea Desemba 26, 2024

Waziri Kombo aliwasili ubalozini hapo Desemba, 31, 2024 na kupokewa na Balozi wa India nchini, Mhe. Bishwadip Dey.

Balozi Kombo aliwasilisha salamu za pole kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo alimweleza Hayati Manmohan kama kiongozi mahiri aliyeimarisha uhusiano mzuri na Tanzania katika mihula miwili ya utawala wake kuanzia mwaka 2004 hadi 2014.

Katika kipindi hicho cha ungozi wake Hayati Manmohan aliwahi kufanya ziara nchini Tanzania wakati wa Serikali ya awamu ya nne iliyokuwa ikiongozwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete..

Post a Comment

0 Comments