SHIRIKA la Watoto Duniani (UNICEF) kwa kushirikiana na Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wametoa ufadhili wa shilingi milioni 93.9 kwa Halmashauri ya Kaliua kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu.
Kupitia ufadhili huo Shule ya Sekondari Kasungu imepata ufadhili wa ujenzi wa maabara ya sayansi kwa gharama ya shilingi milioni 25.7 wakati Shule ya Msingi Kazaroho imepata ufadhili wa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na kukarabatiwa vyumba viwili vya madarasa kwa gharama ya Shilingi milioni 68.2.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kasungu, Bw. Khamis Hamadi Juma na Mkuu wa Shule ya Msingi Kazaroho Bi. Neema Mbise wamepongeza juhudi hizi, wakibainisha kuwa zimeimarisha mazingira ya kujifunza, kupunguza utoro, na kuinua ufaulu wa wanafunzi.
kupitia ushirikiano huu wa UNICEF na TEA miradi 13 yenye thamani ya shilingi milioni 834.3 imefadhiliwa katika mikoa ya Tabora, Kigoma, na Songwe, ikihusisha ujenzi wa maabara, vyumba vya madarasa, na matundu ya vyoo kwa shule za msingi na sekondari.
Jengo la vyumba vitatu vya madarasa lililojengwa kwa ufadhili wa UNICEF kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA) kwa ajili ya shule ya msingi Kazaroho katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua-Tabora
Timu ya maafisa kutoka UNICEF na TEA ulipotembelea mradi wa maabara ya Sayansi katika shule ya msingi Kazaroho katika Halmashauri ya Wilaya Kaliua-Tabora
Timu ya maafisa kutoka UNICEF na TEA ulipotembelea mradi wa madarasa katika shule ya msingi Kazaroho katika Halmashauri ya Wilaya Kaliua-Tabora
0 Comments