Na Mwandishi Wetu.
Desemba 01 , 2024 - Wafanya Biashara Amos Magaba kutoka Sumbawanga na Benson Kilalika kutoka Moshi , wameipongeza Kampuni ya MMI Steel Mill Ltd kwa kutimiza miaka 30 ya Uzalishaji wa Bidhaa zenye Ubora wa Hali ya Juu , Wateja hao ambao ni wawakilishi wa wafanyabiashara wa Bidhaa za Kampuni iyo wameyasema hayo katika Hafla fupi ya kuadhimisha miaka 30 , Hafla iliyojumuisha wadau na wafanya kazi wa Makampuni ya Motisun Group .
" Serikali imekuwa na Mchango mkubwa kwetu kwa sababu ni mdau wetu mkubwa kuna miradi mingi ya serikali tunafanya ambayo ni takribani asilimia 70 , lakini pia serikali imekua msitari wa mbele kutatua changamoto zetu hasa zile ambazo zinaihusu moja kwa moja tumekuwa na mahusiano mazuri na serikali na ndio maana tumeweza kuvuka mipaka na kuwa na Viwanda nje ya Nchi kama vile Msumbiji , Zambia na Uganda " alisema Bw. Singh
Naye Afisa Masoko Mkuu wa Makampuni yote ya Motsun Group Bw. Erhard Mlyansi amesema sambamba na kusherehekea miaka 30 ya ukuaji wa MMI Steel na Wateja na wadau wao , wametumia Hafla iyo kumkumbuka na Kumuenzi Mwanzilishi wa Makampuni ya Motsun Group Marehemu Subhash Motibhai Patel
" Tunamkumbuka Mzee Wetu Marehemu Subhash Motibhai Patel kwa Maono na Ndoto yake aliyotuachia , kwahiyo tunamkumbuka katika kuadhimisha miaka hii 30 kwa mafanikio ambao aliyafanya na kutuachia " amesema Bw. Mlyansi.
Mwenyekiti wa Motisun Group Bw. Pawan Patel akizungumza na wadau na Wafanya kazi Maadhimisho ya Miaka 30 ya MMI Steel .
0 Comments