Meneja wa Bidhaa za Yas, Eginga Mohamed (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi, Chiku Rashid aliyeibuka miongoni mwa washindi wa shilingi milioni moja katika droo ya wiki ya saba wa Kampeni ya Magift ya Kugift. Anayeshuhudia (katikati) ni Meneja wa Wateja Maalum wa Mixx by Yas, Mary Rutta.
Na Mwandishi Wetu.
Kampeni ya Magift ya Kugift inayoendeshwa na Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi wa Yas ikiwa droo ya wiki ya saba wananchi wanaotumia huduma za mtandao huo wameendelea kuneemeka na kampeni hiyo.
Chiku Rashid mkazi wa jijini Dar, ni miongoni mwa washindi nane walioibuka na zawadi mbalimbali katika droo ya saba yeye akiondoka na shilingi milioni moja ambayo amesema itamsaidia kuboresha mtaji wake wa kuuza nguo.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya kiasi hicho, Chiku amesema zawadi hiyo kwake imekuwa kama ‘sapraiz’ kwani hakuitegemea hivyo itaboresha biashara yake ya nguo hususan kipindi hiki cha sikukuu ambapo biashara hiyo ndiyo msimu wake.
“Nawashauri watumiaji wenzangu wa simu kutumia mtandao wa Yas kujipatia huduma mbalimbali kama vile kununua vocha, vifurushi kufanya miamala kwa kutumia Mixx by Yas ili nao waweze kuibuka washindi kama mimi.” Alisema Chiku.
Akizungumza baada ya kumkabidhi mshindi huyo mfano wa hundi, Meneja wa Bidhaa za Yas, Eginga Mohammed amewataka watumiaji wa simu kutumia mtandao wa Yas kwa huduma mbalimbali kama vile kununua vifurushi, kufanya kwa kutumia Mixx by Yas ili waweze kuingia kwenye droo na kujishindia zawadi mbalimbali.
Eginga amesema hii ni wiki ya saba kuchezeshwa droo na bado wiki sita na kuwataka watumiaji wa simu za mkononi kutumia huduma za Yas ili waweze kuibuka na ushindi ambapo kuna zawadi mbalimbali kama vile, simu janja, pesa taslimu shilingi milioni moja, milioni tano, milioni kumi pamoja na zawadi ya gari jipya aina ya Kia Seltos.
Meneja huyo alimalizia kwa kusema wiki ijayo itachezeshwa droo ya nane ambapo anatarajiwa kupatikana mshindi wa gari hilo jipya na la kisasa aina ya Kia Seltos.
0 Comments