Ticker

6/recent/ticker-posts

MAFUNZO YA UFUATILIAJI NA TATHMNI KWA WIZARA, IDARA ZINAZOJITEGEMEA, WAKALA WA SEREKALI NA MASHIRIKA YA UMMA YAFANYIKA JIJINI TANGA


Mwandishi Wetu

Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kupitia kitengo chake maalumu cha ushauri wa kitaalam na kwa kushirikiana na washirika wa chuo kimeendelea kutekeleza makubaliano na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu ya kuimarisha mifumo ya Ufuatiliaji na Tathmini nchini.

Kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Ofisi ya Msajili wa Hazina, Chuo kimeweza kutoa mafunzo ya awamu ya kwanza (Level 1) kwa siku 3 na kuwashirikisha watumishi wa Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala wa Serikali na Mashirika ya umma kuanzia tarehe 02 hadi 04 na 11 hadi 13 Disemba, 2024 katika ukumbi wa New Kiboko Hall Jijini Tanga.

Akiahirisha mafunzo hayo Afisa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw.Charlton Charles Meena amewataka washiriki wote wa mafunzo kwenda kuwa walimu kwa watumishi wengine, pia amesisitiza kwa mshiriki yeyote alieshiriki mafunzo kwa awamu ya kwanza ni vema wakashiriki awamu zote tatu ili kuwa na uwelewa mzuri wa uratibu wa shughuli za Ufuatiliaji na Tathimini za kazi za serikali.
Mafunzo yameshirikisha watumishi wa umma zaidi ya 200, na yamewawezesha washiriki kujifunza kutofautisha na kutumia ipasavyo aina tofauti za Ufuatiliaji na Tathmini, kuamua jinsi ya kufuatilia na kutathmini miradi, mipango ya kimaendeleo au sera, ikiwa ni pamoja na kuweka bayana matokeo muhimu katika ngazi ya programu kwa kutumia mfumo wa kimantiki (Logical Framework) au miundo ya nadharia ya mabadiliko (Theory of Change).

Aidha mafunzo hayo yamelenga kuwasaidia kuunda viashiria sahihi (SMART), kwaajili Ufuatiliaji na Tathmini, kutumia zana mbalimbali za Ufuatiliaji na Tathmini kwaajili ya ukusanyaji na uchanganuzi wa takwimu, kubuni na kusimamia Tathmini kwa kutumia kanuni za Kiafrika za Tathmini na vigezo vya OECD-DAC na kuandaa ripoti bora za Ufuatiliaji na Tathmini kwaajili ya matumizi ya Serikali, Idara, Wizara, Mashirika na Wakala za Serikali.
Aliongezea kuwa kutokana na umuhimu wa mafunzo hayo, Chuo Kikuu Huria kitaendelea kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, pamoja na Msajili wa Hazina kuandaa awamu nyingine ya mafunzo ya awamu ya kwanza ili kuweza kuzifikia baadhi ya Wizara, Idara zinazojitegemea, mashirika na wakala za serekali ambazo zilishindwa kuleta watumishi kwenye awamu hii ya kwanza ya mafunzo.

Pia alisisitiza kuwa ni vyema kukawa na uelewa kuwa baada ya awamu ya kwanza, kutakua na awamu ya pili na ya tatu ambazo kwa Pamoja, zitawezesha watumishi kubobea katika eneo la Ufuatiliaji na Tathmini wa shughuli za Serikali na hivyo kuboresha utendaji kazi wa serikali na utoaji huduma kwa wananchi.

Post a Comment

0 Comments