Desemba , 06 , 2024 : Kampuni ya Mawasiliano ya YAS ( zamani Tigo ) , imekabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi Kampeni ya “Magift ya kugift” kwa wiki ya 4 ambapo kati ya washindi hao baadhi wamejishindia kiasi cha Shilingi Milioni 1 kila mmoja na zawadi za simu
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo kwa washindi Bi. Edwardina Mgendi - Mkurugenzi wa Masoko Yas, amesema anayofuraha kuona wanakabidhi zawadi kwa washindi kwa wiki ya nne nakudai kuwa hii ni sehemu ya utaratibu wao kutoa zawadi mbalimbali ikiwemo pesa taslimu na zawadi nyinginezo katika kipindi hiki cha kuelekea siku kuu za mwisho wa mwaka.
Bi. Mgendi amesema Watanzania bado wana nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali kila Siku na Kila Wiki pamoja na zawadi kubwa ya Gari , kinachotakiwa ni kufanya miamala kwa wingi kupitia Mixx by Yas maana bado Wiki Tisa.
0 Comments