Washiriki wa mafunzo katika picha ya pamoja na wadau wanaoendesha kampeni dhidi ya vitendo vya kupinga ukatili wa kijinsia wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika hoteli ya Kitopela.
Washiriki wa mafunzo katika picha ya pamoja na wadau wanaoendesha kampeni dhidi ya vitendo vya kupinga ukatili wa kijinsia wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika hoteli ya Kitopela.
Mkufunzi wa nishati kutoka kampuni ya Taifa Gas ambayo ni mdau katika kampeni hii, Praygod Ole Naiko akitoa mafunzo ya matumizi ya nishati salama ya kupikia.
Mkufunzi wa nishati kutoka kampuni ya Taifa Gas ambayo ni mdau katika kampeni hii, Praygod Ole Naiko akitoa mafunzo ya matumizi ya nishati salama ya kupikia.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda ya kipolisi Wilaya ya Msalala SSP Elias Zabroni Masome na timu yake wakiendesha mafunzo kwa walimu Wanawake na mama lishe.
Mafunzo kwa walimu Wanawake na mama lishe yakiendelea
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada.
***
-Pia wapatiwa elimu ya matumizi ya Nishati safi
Kampeni ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia inaendelea ambapo wadau wanaoshirikiana na Barrick wanaendelea kutoa elimu dhidi ya vitendo hivyo sambamba na elimu ya matumizi ya nishati safi katika mikoa mbalimbali nchini.
Katika maadhimisho hayo yanayoendelea Barrick na washirika wake wanaendesha shughuli mbalimbali za kutoa elimu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia sambamba na kutoa mafunzo ya matumizi na nishati safi za kupikia na kugawa majiko ya gesi.
Washirika wa Barrick katika maadhimisho ya mwaka huu ni Jeshi la Polisi kupitia madawati ya kijinsia, Halmashauri za wilaya,mashirika yasiyo ya kiserikali ya VSO, LCF, Jadra, Hope for the Girls and Women (HGWT) , kampuni ya wanasheria ya Bowman na kampuni ya uzalishaji na usambazaji nishati ya gesi nchini ya Taifa Gas.
Akiongea katika hafla ya kufungua mafunzo hayo wilayani Kahama Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda ya kipolisi Wilaya ya Msalala SSP Elias Zabroni Masome amewataka wanajamii wote kushiriki katika mapambano ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia, ukiwemo ukeketaji wasichana pamoja na kuwatumikisha watoto wadogo kazi za Shambani na majumbani badala ya kuwapitia haki yao ya msingi ya kuwapeleka shule.
Aliongeza kuwa Jeshi la Polisi wilaya ya Msalala limejipanga Kikamilifu kukamata na kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya mtu yoyote atakaebainika kujihusisha kwa namna yoyote kumfanyia mwenzake vitendo vya Ukatili wa Kijinsia .
Akizungumza niaba ya Meneja Mgodi wa Barrick Bulyanhulu ,Afisa Mwandamizi wa mahusiano ya Jamii, Zuwena Senkondo, alisema Barrick itaendelea kushirikiana na Serikali na wadau wengine kwenye kampeni mbalimbali nchini pamoja na pampja na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kijamii.
Pia Washirika walipatiwa mafunzo ya matumizi ya nishati salama kutoka kwa mkufunzi wa nishati kutoka Taifa Gas ambayo ni mdau katika kampeni hii, Praygod Ole Naiko ambaye alisema kuwa kampuni hiyo iko mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za Serikali za kuhimiza jamii kutumia nishati safi ya kupikia kwa lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira.
Kupitia kampeni hii Wanawake kutoka sehemu mbalimbali nchini wanaendelea kunufaika kwa kupatiwa elimu ya matumizi ya nishati salama ya kupikia sambamba na kugawiwa majiko na mitungi ya Gesi kutoka kampuni ya Taifa Gas.
Mama Lishe na Walimu ambao wamehudhuria mafunzo hayo wameshukuru Taifa Gas na wadau wake kwa kuwa elimu ya matumizi ya nishati safi ni muhimu kwao kama sehemu ya jamii pia majiko ya kisasa yanawasaidia kuongeza tija katika shughuli zao sambamba na kuwapunguzia adha ya kutumia nishati za kuni na mkaa.
0 Comments