Ticker

6/recent/ticker-posts

WANAHARAKATI WA JINSIA WAIOMBA SERIKALI KUWEKA MKAZO KATIKA ELIMU YA SAYANSI NA KUPAMBANA NA MFUMO DUME

WANAHARAKATI wa Jinsia na Maendeleo wameishukuru serikali kwa juhudi zake ambazo zimezaa matunda, hasa katika kuboresha huduma za afya kwa mama na mtoto, ambapo watoto chini ya miaka mitano sasa wanapata huduma bure. Hii ni baada ya miaka 30 tangu mkutano wa Beijing, ambao ulianzisha mikakati ya kukuza haki za wanawake na watoto.

Akizungumza kwenye Semina za Jinsia na Maendeleo zilizofanyika kwenye Ukumbi wa TGNP- Mtandao Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Novemba 2024, Mkurugenzi wa Shirika la Macho kwa Jamii, Theresia Lihanjala, ameeleza kuwa serikali imefanya juhudi kubwa katika kuhakikisha kuwa vitanda vya kutosha vinapatikana hospitalini na wanawake wanapata huduma bora za afya.

Aidha Lihanjala ameiomba serikali kusimamia kikamilifu haki ya mtoto wa kike kupata Elimu hasa kwemye masomo ya Sayansi kwani imezoeleka kuwa mtoto wakike anapoanza kusoma kuanzia shule ya msingi hadi sekondari ameonekana kufanya vizuri lakini jambo la kushangaza anapohitimu anapangiwa fani za sanaa.

Sambamba na hayo ameeleza changamoto nyingine ambayo wanatamani ikomeshwe ni uwepo wa mfumo dume katika suala la uongozi kwani mwalimu mwanamke amekuwa akinyimwa nafasi ya uongozi wa shule kutokana na dhana kwamba atabeba ujauzito na kuacha shule bila uongozi.

Kwa upande wake,Mwanaharakati wa Jinsia na Maendeleo, Wenseslaus Kidakule ameshauri kuwa ili kuwa na haki sawa ni lazima kundi la wanawake lihusishwe bila kuliacha nyuma na kulishirikisha katika vipaumbele vya kiuchumi pamoja na masuala ya uongozi.

Aidha Wenseslaus ameeleza kuwa serikali ikishirikiana na taasisi zisizo za kiserikali NGOS katika ngazi mbalimbali za maamuzi na kwenye masuala ya kisera na kisheria zitasaidia kuleta suluhisho la kudumu 

Post a Comment

0 Comments