Na Munir Shemweta, WANMM Kigoma
Tanzania na Burundi zimetiliana saini ya makubaliano ya uimarishaji mpaka wa kimataifa baina ya nchi hizo.
Makubaliano hayo yamefikiwa jana mara baada ya kukamilika kwa Kikao cha Kamati ya Pamoja cha Wataalamu (JTC) kati ya Tanzania na Burundi kilichofanyia kwa siku tano mkoani Kigoma.
Utiaji saini makubaliano hayo umefanywa kati ya kiongozi wa timu ya Tanzania ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi idara ya Upimaji na Ramani Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Samwel Katambi na Meja Jenerali Mbonimpa Maurice ambaye ni kiongozi wa timu ya wataalamu kutoka nchini Burundi.
Akizungunza wakati wa utiaji saini makubaliano hayo, mkuu wa timu ya Tanzania Bw. Samwel Katambi amepongeza michango ya washiriki wa kikao cha pamoja cha wataalamu ambapo amesema, michango hiyo imelenga kujenga uhusiano mzuri wa nchi mbili za Tanzania na Burundi sambamba na kuimarisha mipaka ya nchi hizo.
Bw. Katambi ametaka yale waliyokubaliana kwenye kikao hicho cha JTC yatekelezwe ili kufikia malengo na hatimaye kukamilisha kazi ya uimarishaji mpaka wa kimatifa kama ilivyopangwa.
Naye kiongozi wa timu ya wataalamu kutoka nchini Burundi Meja Jenerali Mbonimpa Maurice amewashukuru washiriki wa kikao hicho cha Wataalamu cha JTC kwa kumalisha kazi kwa pamoja, kazi aliyoieleza kuwa imekuwa nzuri na ya mafanikio.
Kwa mujibu wa Meja Jenerali Mbonimpa, serikali ya Burundi iko tayari kufanyia kazi waliyokubaliana ikiwemo mpango kazi wa utekelezaji kazi ya uimarishaji mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Burundi.
Wakati wa kikao cha Kamati ya Pamoja cha Wataalamu (JTC), wajumbe walipata fursa ya kutembelea Mto Malagarasi ambao ni sehemu ya mpaka wa kimataifa kati ya nchi hizo mbili sambamba na vijiji vya Bukililo na Nyakayenzi upande wa Tanzania na kijiji cha Kamusha nchini Burundi kwa lengo la kujionea hali halisi ya maeneo hayo.
Lengo la kutembelea maeneo hayo ya mpaka ni kuwezesha kamati ya JTC Kuandaa bajeti na mpango kazi wa uimarishaji mpaka wa kimataifa baina ya Tanzania na Burundi.
Zoezi la uimarishaji mipaka ya kimataifa ni utekelezaji wa makubaliano ya umoja wa Afrika kuwa ifikapo mwaka 2027 mipaka baina ya nchi za afrika iwe imeimarishwa.
Kiongozi wa timu ya wataalamu wa Tanzania ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi idara ya Upimaji na Ramani Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Samwel Katambi (kushoto) pamoja na Meja Jenerali Mbonimpa Maurice ambaye ni kiongozi wa timu ya wataalamu kutoka nchini Burundi wakisaini Hati ya Makubaliano ya Uimarishaji mpaka wa kimataifa kati ya nchi zao mara baada ya kumalizka kikao cha JTC kilichofanyika manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma jana.
Kiongozi wa timu ya Tanzania ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi idara ya Upimaji na Ramani Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Samwel Katambi na Meja Jenerali Mbonimpa Maurice ambaye ni kiongozi wa timu ya wataalamu kutoka nchini Burundi wakibadilishana Hati ya Makubaliano ya Uimarishaji mpaka wa kimataifa kati ya Tanzania na Burundi mara baada ya kikao cha JTC kilichofanyika katika manispaa ya Kigoma Ujiji Kigoma jana.
Kiongozi wa timu ya Tanzania ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi idara ya Upimaji na Ramani Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Samwel Katambi (kushoto) pamoja na Meja Jenerali Mbonimpa Maurice ambaye ni kiongozi wa timu ya wataalamu kutoka nchini Burundi wakionesha Hati ya Makubaliano ya Uimarishaji mpaka wa kimataifa kati ya Tanzania na Burundi mara baada ya kusaini makubaliano wakati wa kikao cha JTC kilichofanyika Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma jana.(PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
Kirefu cha JTC ni -Joint Technical Committee
0 Comments