Ticker

6/recent/ticker-posts

KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA TVLA KWA KUZALISHA CHANJO

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo chini ya Mwenyekiti wake, Mhe. Deodatus Mwanyika imeipongeza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kwa uzalishaji wa chanjo za mifugo ambazo zinatumika kuboresha afya za mifugo hapa nchini.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Mhe. Dedatus Mwanyika kwa niaba ya kamati hiyo walipotembelea Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) iliyopo Kibaha, Mkoa wa Pwani Novemba 12, 2024.

Kwa upande wake Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Alexander Mnyeti amesema mipango ya Wizara ni kuendelea kuhamasisha pamoja na kutoa elimu kwa wafugaji kuhusu umuhimu wa kuchanja mifugo

Aidha, Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya VeterinariT anzania (TVLA), Dkt. Stella Bitanyi amesema kwa sasa wameanza kuwafikia wafugaji moja kwa moja kuwapa elimu ya umuhimu wa chanjo kwa mifugo yao.

Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) ipo chini ya Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) ambapo jukumu lake kubwa ni kufanya tafiti na kuzalisha chanjo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Viwanda Biashara, Kilimo na Mifugo Mhe. Deodatus Mwanyika (Mb) akisalimiana na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Mnyeti (Mb) muda mfupi mara baada ya kuwasili Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) iliyopo Kibaha Mkoa wa Pwani Novemba 12, 2024 alipotembelea Taasisi hiyo kukagua maendeleo ya uzalishaji wa chanjo za Mifugo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Stella Bitanyi akitoa taarifa fupi kuhusiana na utendaji kazi wa Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) kwa kamati ya Kudumu ya Bunge, Viwanda Biashara, Kilimo na Mifugo walipotembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kukagua maendeleo ya uzalishaji wa chanjo za Mifugo Novemba 12, 2024 Kibaha Mkoa wa Pwani.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Mnyeti (Mb) akitoa neno la utangulizi kuwakalibisha wajumbe Kamati ya Kudumu ya Bunge, Viwanda Biashara, Kilimo na Mifugo kwenye Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) walipotembelea Taasisi hiyo kukagua maendeleo ya uzalishaji wa chanjo za Mifugo Novemba 12, 2024 Kibaha Mkoa wa Pwani.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Viwanda Biashara, Kilimo na Mifugo Mhe. Deodatus Mwanyika (Mb) akiangalia chanjo ya Homa ya Mapafu kwa Ngombe (BOVIVAC) zinazozalishwa na Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) Novemba 12, 2024 alipotembelea Taasisi hiyo kukagua maendeleo ya uzalishaji wa chanjo za Mifugo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Stella Bitanyi (Kushoto) akitoa maelezo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Viwanda Biashara, Kilimo na Mifugo kuhusiana na taratibu za uzalishaji wa chanjo unaofanywa na Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) walipotembelea Taasisi hiyo kukagua maendeleo ya uzalishaji wa chanjo za Mifugo Novemba 12, 2024 Kibaha Mkoa wa Pwani. Wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Viwanda Biashara, Kilimo na Mifugo Mhe. Deodatus Mwanyika (Mb) na wa pili kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Mnyeti (Mb).
Afisa Mifugo Mtafiti wa Wakala ya Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Bwa. Joseph Kabadi akitoa maelezo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Viwanda Biashara, Kilimo na Mifugo kuhusiana na uzalishwaji wa chanjo za magonjwa ya virusi zinazozalishwa na Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) Novemba 12, 2024 walipotembelea Taasisi hiyo kukagua maendeleo ya uzalishaji wa chanjo za Mifugo. Wa kwanza kushoto niNaibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Mnyeti (Mb).
Mtaalamu wa Maabara wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Bi. Shukuru Nganga akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Viwanda Biashara, Kilimo na Mifugo kuhusiana taratibu za uzalishaji wa chanjo ya Homa ya Mapafu kwa Mbuzi (CAPRIVAC) zinazozalishwa na Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) walipotembelea Taasisi hiyo kukagua maendeleo ya uzalishaji wa chanjo za Mifugo.

Post a Comment

0 Comments