Ticker

6/recent/ticker-posts

Elimu ya Uzalishaji Mbegu Bora za Mpunga Yatolewa Bagamoyo

Wadau wa masuala ya kilimo wametakiwa kujitokeza kutoa elimu  ya uzalishaji mbegu kwa wakulima wa mpunga  ili kuondokana na changamoto ya uzalishaji mbegu nchini  pamoja na kuongeza uzalishaji wa zao hilo nchini.
 
Akizungumza  Novemba, 4 2024 wakati wa kufungua mafunzo ya siku tatu ya uzalishaji wa mbegu za ubora wakuazimia (UKU) za mpunga iliyofanyika wilayani Bagamoyo iliyoandaliwa na Taasisi ya  Kimataifa ya Utafiti wa Mpunga( IRRI) na kuvikutanisha vikundi vya uzalishaji mbegu  kutoka mikoa mbalimbali ,Mkuu wa Idara ya Kilimo na Mifugo Wilaya ya Bagamoyo Gerald Mwamuhamila alisema ni wakati wa wadau sasa kujitokeza na kuokoa sekta hiyo kwakufundisha wakulima kutengeneza mbegu ambazo zitazalisha mpunga bora.
 
"Lengo la mafunzo hayo  ni kwa ajili ya kuzalisha Mbegu za kuazimia ubora na kufanya hivyo ni kutatua changamoto  ya upungufu wa mbegu za mpunga ambayo ipo inawakabili wakulima mbalimbali.

"Kupitia mafunzo haya maanaake wakulima hawa watakuwa wamerudi kwenye maeneo yao  watakuwa na jukumu la kuzalisha mbegu zilizo bora,ili kufanikisha hilo tunatoa kwa wadau wanaofanya kazi kama IRRI watusaidie kupanua wigo za taasisi za uzalishaji  kwa kutoa elimu kwa wakulima  mbalimbali  wa mazao mengine  ili wapate wawezeshaji ili kuondokana na changamoto ya mbegu nchini,"alisema Mwamuhamila.
 
Alisema wazalishaji wa mazao yakiwemo mpunga ni wengi nchini lakini suala la mbegu zenye ubora limekuwa changamoto na badala yake watu wengi wamekuwa wakizalisha mpunga kwa mbegu zinajirudia  na kusababisha uzalishaji  unakuwa chini tofauti na mwanzo.

"Mfano kwenye kikundi cha kuzalisha mbegu Bagamoyo kwa sasa wanazalisha tani mbili na nusu kwa hekta moja wakati mahitaji halisi  kwa mkulima ambaye amezalisha na kuzingatia utaratibu ikiwemo mbegu bora uzalishaji unapaswa kuwa ni kuanzia tani nne ndiyo malengo,kupitia mafunzo haya ifikapo mwaka 2025 na mwakani 2030 wanatarajia mkulima kufikisha tani sita kwa hekta moja,"alisema.
 
Alisema jumla ya washiriki 35 walioshiriki mafunzo hayo kutoka katika vikundi 13 vya uzalishaji wa mbegu kutoka Wilaya ya Bagamoyo  wa wawakilishi wa vikundi kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es salaam,  Katavi,Mbeya na mingineyo.

Alisema baada ya mafunzo hayo wanatarajia wakulima hao watakaozalisha mbegu zinakuwa na idhini ya Wakala wa Mbegu nchini (ASA)  pia wanaoruhusu matumizi bora ya mbegu na Taasisi ya Kudhibiti Ubora  wa Mbegu Nchini (TOSCI).

Aliongeza  kuwa kukupitia semina hiyo mbegu zitakazozalishwa zitawafaa wakulima  walioshiriki mafunzo na wengine ambao hawapo hapo na bei yake itakuwa nafuu tofauti  kampuni zingine zinazozalisha mbegu hiyo.

Alisema uzaishaji wambegu pia utasaidia kutatua ukosefu wa chakula na wakulima wataongeza uzalishaji ili waweze kuzalisha ziada  kupata mapato mengine nje ya chakula.

Naye  Afisa Miradi wa Shirika la Maendeleo  ya Kilimo Afrika Mashariki,  Robert Mwalubeke alisema lengo la mafunzo hayo ni kuandaa wazalishaji  mbegu hasa zenye ubora kwakuwa kuna changamoto ya upatikanaji wa mbegu na kuwafikia wakulima kwenye mabonde waliopo.

"Mbegu bora kuwafikia wakulima ilikuwa changamoto  hivyo tunaongeza elimu ya uzalishaji ili mbegu ipatikane kwa wakati sahihi,hapa tunaandaa wazalishaji katika maeneo mbalimbali ili wazalishe mbegu zenye ubora kuwauzia wakulima waliopo maeneo husika,"alisema

Alisema mafunzo hayo yanalenga kuongeza upatikanaji wa mbegu bora kwa  wakulima nchini  na upatikanaji wa mbegu bado hauridhishi.

"Zaidi ya wakulima asilimia 70 wanarudia mbegu na chini ya asilimia 30 wanapanda mbegu mpya hiyo ni fursa,hasara za kurudia mbegu ni pamoja na  mavuno  kuwa madogo kupata mbegu haina ubora na mpunga ukivuna hauna ubora na kupunguza kipato kwa mkulima,"alisema. 

Kwa upande wake  mshiriki kikundu cha Tuinuane Kiuchumi kutoka Rukwa, Neema Japhet alisema wao wanajishughuli na kilimo cha mpunga na kupitia mafunzo hayo wanaamini watafanya kilimo chenye tija zaidi.

Alisema lengo la kushiriki mafunzo hayo  ni kujifunza jinsi ya kuandaa mbegu bora  za  mpunga  hivyo wanatarajia  kuendelea  kutoa elimu  kwa wakulima wa mkoa huo  ili waweze kuzalisha kwa wingi  mbegu.

Post a Comment

0 Comments