NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Benki ya Equity Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Rikolto pamoja na Motley wamekuja na Bajaji ambazo zina chumba maalumu chenye ubaridi kwa ajili ya kuhifadhia mazao ya mbogamboga na matunda kwa lengo la kusaidia kuongeza thamani ya mazao hayo ili kuepusha kuharibika wakati wa kuyasafirisha.
Akizungumza leo Novemba 26,2024 Jijini Dar es Salaam Meneja Kitengo cha Bidhaa na Ushirikiano EQUIT BANK Martine Rajabu amesema kutokana na mbogamboga na matunda kuharibika kabla ya kumfikia mtumiaji walipata wazo ambalo litakuwa ni suluhisho la changamoto hiyo ambapo wameleta Bajaj maalumu kwa ajili ya kubeba mazao hayo.
"Katika bidhaa hizi mboga mboga na matunda yakikaa kidogo tu yanaharibika tukaona tuje na hii bidhaa ambayo ina chumba baridi ambayo itaweza kusafirisha matunda na mbogamboga hadi majumbani vikiwa salama"Amesema.
Martine amesema lengo lao hasa ni kuwapunguzia hasara wakulima na wafanyabiashara wa bidhaa za mbogamboga na matunda ili wakue kiuchumi pamoja na kuwatanulia wigo la kufikia soko kubwa la walaji.
Aidha ameeleza kuwa kutokana na Vijana wengi kutokuwa na uwezo wa kumiliki Bajaj hizo kupitia. bidhaa yao ya kibenki iiitwayo Ufadhili wa amali (Asset financing) inamwezesha kijana kuchangia Asilimia 25 ambapo ataendeleaa kukamilisha hadi kufikia miezi 24.
Kwa Upande wake,Mkurugenzi taasisi ya Rikolto Afrika Mashariki,Kaimu Mbanda amesema taasisi yao imeamua kugharamia Bajaj hizo kwa Asilimia 60 na benki ya Equity yenyewe itatoa mkopo ambapo lengo lao kuu nikuepusha uharibifu mkubwa.
Aidha Mbanda ameeleza kuwa baada ya kugundua zaidi ya Asilimia 40 ya chakula kinapotea njiani kutokana na kutokuwa na uhifadhi mzuri ambapo taasisi yao kwa kushirikiana na wadau wengine wameazimia kuleta teknolojia ambayo itasaidia kupunguza uharibifu wa chakula.
0 Comments