Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI JAFO AZINDUA BODI YA WAKURUGENZI YA FCC.


Waziri wa Viwanda na Biashara Mh.Suleiman Jafo ameitaka Bodi Mpya ya Wakurugenzi wa Tume ya Ushindani( FCC) kufanya vikao vya haraka ili kupitia mambo yote yanayotakiwa kupatiwa ufumbuzi katika masuala ya uwekezaji Nchini.

Waziri Jafo ametoa maelekezo hayo leo Oktoba 4,2024 Jijini Dar es salaam wakati akizindua bodi hiyo,nakusema kuwa bodi hiyo inajukumu kubwa la kumsaidia Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika maono yake yakuvitia wawekezaji na kukuza Uchumi wa Taifa.

Aidha amesema kuwa FCC ni injini ya uwekezaji Nchini,hivyo bodi hiyo mpya itasaidia Wizara ya Viwanda na Biashara katika kuhakikisha Sekta Binafsi inakua kwa kasi nakuleta mchango wa Maendeleo pamoja na kuondoa changamoto ya ajira kwa Vijana.

"Wakati mwingine makampuni ya nahitaji kuungana ,lazima uwepo upembuzi(Analysis ) haraka kuona je Muungano huo una tija kwa Taifa,kama una tija basi mfanye mchakato undelee kwa haraka," amesema Waziri Jafo

Nakuongeza kuwa "Sekta binafsi ndio suluhisho la kujibu mahitaji ya ajira kwa Vijana wanaohitimu kila Mwaka ,na jukumu hili tumepewa sisi Wizara ya Viwanda na Biashara,naomba sana FCC mfanye kazi yenu kwa uadilifu na uaminifu mkubwa.

Aidha Waziri Jafo amewashauri watendaji wa FCC kufanya kazi kwa kuzingatia mabadiliko ya sheria katika kufanya tathmini ya namna makampuni yanavyoweza kuungana ili kuleta tija katika ushindani kibiashara.

Hata hivyo Waziri huyo wa Viwanda na Biashara amewataka watendaji wa Tume ya Ushindani kutoa ushirikiano wa dhati kwa Bodi ya Wakurugenzi ili iweze kufanya kazi nakufikia malengo waliyojiwekea,nakwamba bodi hiyo isipofanya kazi zake vizuri inaweza kuiyumbisha Serikali.

Awali Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa maono ya kuweka mazingira rafiki na tulivu ya ufanyaji Biashara Nchini.

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya FCC Dkt.Aggrey Mlimuka amemhakikishia Waziri Jafo kutekeleza maelekezo yote aliyoyatoa kwa Bodi hiyo.

"Mheshimiwa Waziri tutayafanya yote ukiyotuelekeza,na Bodi hii natumaini itakua na weledi Mkubwa katika kumsaidia Rais Wetu mpendwa kuvutia wawekezaji na kuleta ushindani katika tiafa letu.

Post a Comment

0 Comments