Ticker

6/recent/ticker-posts

Serikali Yasisitiza Uhifadhi wa Ziwa Tanganyika

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis ametoa wito kwa Nchi Wanachama wa Ziwa Tanganyika kuendelea kulinda ziwa hili ili lisaidie katika shughuli za kijamii.

Ametoa witi huo wakati akiwasilisha taarifa wakati wa Mkutano wa Tatu wa Mawaziri wa Nchi za Ziwa Tanganyika zinazoundwa na Tanzania, Zambia, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wa kujadili kuongezeka kwa kina cha ziwa hilo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Oktoba 04, 2024.

Mhe. Khamis amesema kuwa zipo hatua mbalimbali ambazo Serikali ya Tanzania inachukua kuhakikisha Ziwa Tanganyika linakuwa salama kimazingira.

Amesema Serikali imekuwa ikihimiza wananchi hususan wanazunguka ziwa hilo kupanda miti katika maeneo yanayolizunguka ili kupunguza mmomonyoko wa udongo.

Halikadhalika, Naibu Waziri Khamis amesema ili kukabiliana na changamoto ya uvuvi usio endelevu na zisizo rasmi ambazo kwa kiwango kikubwa zinachangia katika uharibifu wa mazingira.

“Kama nchi tunasimamia Sheria za Uvuvi ili wananchi wetu waweze kuzifuata ili lengo la kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi litimie na hatimaye maji haya ya ziwa yawe yanapungua siku hadi siku,“ amesisitiza.

Post a Comment

0 Comments