Ticker

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YABAINISHA MIKAKATI YA KUWEZESHA VIJANA KIUCHUMI TANZANIA BARA NA ZANZIBAR

Serikali imeendelea kuweka mikakati endelevu ya kuwawezesha vijana nchini ili waweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji mali na kukuza uchumi wa Taifa.

Hayo yameelezwa wakati wa Kongamano la Vijana lililofanyika leo Oktoba 10, 2024, jijini Mwanza.

Akizungumza Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Mhe.Tabia Maulid Mwita amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Mapinduzi Zanzibari inayoongozwa na Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi zimekuwa zikichukua hatua za kuwashirikisha vijana katika nyanja mbalimbali kwa lengo la kuwaendeleza kiuchumi.

Awali akizungumza Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amesema Serikali imeonyesha dhamira ya kuwawezesha vijana kwa kutoa mikopo ya asilimia 10, ambayo ni sehemu ya mpango wa kuwezesha vijana nchini.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ametoa wito kwa vijana na wananchi wa Mkoa wa Mwanza na Mikoa ya Jirani kutembelea mabanda ya maonesho ya wiki ya vijana yanayoendelea viwanja vya furahisha ili kujionea shughuli za kibunifu za vijana.

Wiki ya Vijana uadhimishwa kila mwaka tarehe 8 hadi 10 Oktoba, ambapo kwa Mwaka huu 2024 kauli mbiu ya maadhimisho hayo ikiwa ni “Vijana na Matumizi ya Fursa za Kidijitali kwa Maendeleo Endelevu”.

Post a Comment

0 Comments