Ticker

6/recent/ticker-posts

PROF. SEDOYEKA AMALIZA UTATA JUU YA TUHUMA ZILIZOKUWA ZINAMKABILI


Na Imma Msumba : Dodoma

Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma octoba 17 imemaliza kusikiliza malalamiko dhidi ya tuhuma zinazomkabili Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Prof.Emilian Sedoyeka, anayetuhumiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi hiyo, kinyume na kanuni na taratibu za maadili ya uongozi wa umma ambapo amekana tuhuma zote.

Akisoma malalamiko yanayomkabili Prof. Sedoyeka Jijini Dodoma mbele ya Rose Teemba Mwenyekiti wa Baraza la Maadili ,Wakili wa Serikali Emma Gelani amesema malalamiko hayo yaliwasilishwa Septemba 15,2024 ambayo kiongozi huyo anatuhumiwa kwa kushindwa kutimiza matakwa ya sheria ya maadili ya umma kifungu cha 6(1)c na kifungu cha 12(1).vya sheria ya maadili ya uongozi wa umma.

Wakili Mkuu wa serikali Emma Gellan, amesema mlalamikiwa anatuhumiwa na mashtaka manne ikiwamo kumpandisha cheo Bw. Hakimu Ndatama, kutoka Afisa Rasilimali kuwa Mkuu wa sehemu ya rasilimali watu, kabla ya kukamilika kwa uhamisho wa mtumishi huyo na bila kuwa na sifa.

Malalamiko hayo ni pamoja na Tuhuma ya kuwa na ukaribu na Bw. Hakimu Ndatama na uhamisho wake kurudi IAA pindi aliporejea kuwa Mkuu wa Chuo.

Profesa sedoyeka amesema Uhamisho wa Bw. Ndatama kwenda Wizara ya Maliasili na Utalii ulifuata taratibu zote za kisheria na kufuatia mahitaji ya kikazi, Chuo kiliandika kwenda Wizara ya Maliasili na Utalii ya kuomba Bw. Ndatama arejeshwe ambapo hilo la kuomba arejeshwe lilifanyika kabla ya yeye kurejea IAA kutokana na mahitaji ya kikazi. Alisema

Aidha ametolea ufafanuzi Tuhuma kuhusu Uteuzi wa Bw. Hakimu Ndatama kuwa Mkuu wa Sehemu ambapo amesema tuhuma ya kutekeleza uteuzi wa Bw. Hakimu Ndatama na mgongano wa maslahi ni kwamba uteuzi huo ulikuwa na msingi mzuri unaozingatia uwezo na ufanisi wake katika utekelezaji wa majukumu yake.

"Nilizingatia sifa za Bw. Ndatama na uwezo wake wa kuchangia maendeleo ya IAA. Nikiwa na dhamira ya kulinda maslahi ya taasisi na kuhakikisha tunapata watu wenye uwezo wa kuchangia katika malengo yetu ya taasisi". Amesema

Bw. Ndatama si ndugu yangu, si kabila langu, si dini yangu, si rafiki yangu na wala hakuna chochote kinachoniunganisha naye. Sina maslahi naye kwa namna yoyote ile". Ameongeza

Tuhuma nyingine ni Zabuni ya Viti na Meza vya Wanafunzi kwa Kampasi ya Babat ambapo Kwa Kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi ya Umma, Na. 7 ya mwaka 2013), inampa mamlaka Afisa Masuuli kukataa kuendelea na zabuni ama kurejesha zabuni kwenye Bodi ya Zabuni.

"vifungu hivyo vimefafanua kwamba atakapofanya hivyo ataeleza sababu na kupata idhini ya Bodi ya zabuni (Tender Board). Ninaweka wazi msimamo wangu kwamba nilifuata taratibu zote na sikuvunja sheria bali nilikuwa nikitekeleza majukumu yangu kwa mujibu wa Sheria". Ameeleza

"kama kiongozi mwaminifu kwa nchi yangu, nimekuwa makini kuhakikisha taasisi inapata bidhaa bora kwa njia za uwazi na kwa gharama nafuu kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma". Amesema

"Katika mazingira yote ya manunuzi ya umma, dhamira yangu kama Afisa Masuuli ni kuongeza wigo wa ushindani kwa lengo la kupata thamani halisi ya pesa za Umma (value for money). Hivyo nimekuwa na msimamo wa uwazi na kuzingatia taratibu zinazotakiwa, kwa lengo la kulinda maslahi ya taifa na kuimarisha taasisi ili iweze kufikia malengo yake ya kutoa elimu bora kwa jamii". Amesema

Kadhalika Tuhuma kuhusu Uhamisho wa Ndani wa Mtumishi Bw. Robert Mwitango Kwa ujumla uhamisho wa ndani wa watumishi hufanywa kwa lengo la kuboresha ufanisi wa kiutendaji wa taasisi.

"Katika Mwaka wa 2023/2024 Idara ya Maktaba ilipanga kutekeleza shughuli mbalimbali zikiwemo zile ambazo kwa uhalisia wake zilihitaji msaada wa karibu wa kitengo cha Manunuzi ya Umma, kama Stock taking, Asset Verification” na Ununuzi mkubwa wa vitabu kwa mkupuo.". Amesema

"Nilipotathmini ukubwa wa majukumu hayo, unyeti wake na namna yanavyohitaji utaalamu wa manunuzi ya umma, niliamua mtumishi mmoja afanyiwe uhamisho wa ndani kutoka kitengo cha Manunuzi kwenda Idara ya Maktaba". Ameongeza

Baada ya kusomewa malalamiko hayo mlalamikiwa alikana makosa yote huku upande wa serikali ukiwasilisha mashahidi Wanne.

Awali akitoa ushahidi wake mbele ya Baraza la maadili kwa upande wa Mlalamikaji amesema walianza kuchunguza malalamiko hayo machi hadi mwanzoni mwa Novemba mwaka jana.

Amesema baada ya kufanya uchunguzi wa kina walibaini kuwa mlalamikiwa alifanya matukio yote manne ikiwa ni kinyume na maadili ya viongozi wa umma.

Katika malalamiko hayo upande wa Mlalamikaji baada ya kuwasilisha vielezo ambayo vilikusanywa kwa wakati tofauti tofauti ambapo Profesa Sodeyeka alikubali vitumike.

Awali katika maswali ya papo hapo Profesa Sodeyeka alimuhoji shahidi huyo kuwa kuna ubaya wowote Mkuu wa Taasisi kumbadilishia Mtumishi majukumu yake.

Akijibu swali hilo shahidi wa Mlalamikaji amesema kuna tofauti inaruhusiwa lakini uwe ndani ya msingi wa kazi yake

Post a Comment

0 Comments