Ticker

6/recent/ticker-posts

PROF. NOMBO AZINDUA MIONGOZO MINNE YA USIMAMIZI WA UTAFITI NA UBUNIFU COSTECH

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) Prof. Carolyne Nombo amesema, Serikali kupitia Mradi wa Mageuzi ya Kiuchumi Elimu ya Juu (HEET), imewekeza jumla ya trilioni 1.1 katika miundombinu ya Elimu, vifaa vya kisasa vya kufundishia, kuimarisha ushirika baina ya Vyuo Vikuu na Sekta ya Viwanda, pamoja na masuala ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu. 

Ameongea hayo wakati wa uzinduzi wa miongozo minne ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu pamoja na uzinduzi wa huduma ya ziada kwa vyuo vya ualimu kwa njia ya video call, kupitia mradi wa Mageuzi ya Kiuchumi kwa Elimu ya Juu (HEET) uliofanyika tarehe 04 oktoba, 2024. ofisi za COSTECH jijini Dar Es Salaam.

Prof. Nombo ameeleza kuwa miongozo hiyo ni sehemu ya zao la mradi wa HEET, na tunaamini baada ya uzinduzi tutakua tumeingia katika mifumo ya utendaji wetu na namna ambavyo tutaimarisha na kuratibu masuala yote ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu.

" Utafiti na Ubunifu ni nyenzo katika kuchangia maendeleo ya Kiuchumi na kijamii, nchi zote zilizoendelea duniani zimefanikiwa kutokana na uratibu na uwekezaji madhubuti katika masuala ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu" amesema Prof. Nombo.

Aidha, Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuwekeza zaidi katika kuimarisha maendeleo na mchango wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ili kustawisha uchumi wa viwanda na maisha ya watanzania kwa ujumla. Hivyo kupitia ushirikiano wa taasisi za elimu ya juu na Sekta za viwanda, kuhakikisha inaboresha matokeo yenye tija  ya utafiti na ubunifu, miongozo minne iliozinduliwa rasmi ni hatua kubwa katika kuimarisha mifumo ya usimamizi wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu nchini, amesema Prof. Nombo.

"Miongozo hii ni nyenzo muhimu sana kwa watunga Sera, Taasisi za Elimu ya Juu, viwanda na jamii ya watanzania kwa ujumla wake, Wzara ya Elimu , Sayansi na Teknolojia imejiwekea malengo makubwa ya kuboresha Elimu na kuimarisha Sayansi na Teknolojia ili kuchochea maendeleo ya Taifa letu" amesema Prof. Nombo.

Kwa upande mkurugenzi mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) dkt. Amos Nungu amesema tume inatekeleza mradi wa HEET kupitia maeneo sita ambayo yote yanaongelea katika ujenzi wa miundombinu ya Sayansi, teknolojia na ubunifu, kutunza na kuendeleza uwezo wa watafiti na wabunifu, kujenga uhusiano katika sekta binafsi na taasisi za Utafiti na maendeleo ya juu, kuboresha miundombinu ya kisasa ya tehama pamoja na kukuza uwezo endelevu na kusimamia tafiti na bunifu nchini.

" tunashirikiana na wadau mbalimbali kama vyuo vikuu na Sekta za utafiti maendeleo na Sekta binafsi katika kutayarisha miongozo hii, na pia ni nyenzo muhimu kwa watafiti, wabunifu na taasisi za umma na inalenga kukuza ubora wa utafi na ubunifu na maendeleo endelevu" amesema dkt. Nungu.

Dkt. Nungu amehitimisha kwa kusema,
miongozo hii inalenga kuimarisha uratibu katika sekta ya utafiti, ubunifu, na teknolojia nchini Tanzania, ambapo kila mwongozo unalenga kutoa mwelekeo thabiti kwa sekta ndani ya ekolojia ya ubunifu na utafiti ili kuhakikisha tunafikia malengo yetu ya kitaifa ya kiuchumi na kijamii.

Post a Comment

0 Comments