Ticker

6/recent/ticker-posts

NCHIMBI: AMANI IWE KIPAUMBELE CHETU WATANZANIA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amesema amani na mshikamano wa Watanzania unapaswa kuwa mojawapo ya vipaumbele kwa kila Mtanzania.

Balozi Nchimbi amesema kuwa wasisi wa Taifa la Tanzania na wazee walifanya kazi kubwa katika kuweka misingi ya kulinda na kutunza amani ya nchi, wakitumia hekima na uzoefu ili kuhakikisha kuwa jamii ya Watanzania inakuwa na mshikamano siku zote.

“Ni jukumu letu sasa kuendeleza amani hiyo na thamani yake kwa ajili ya vizazi vijavyo. Ni muhimu kutunza umoja wetu na kushirikiana kwa pamoja. Tunapaswa kudumisha na kujenga mazingira ya amani na ushirikiano. Umoja ni nguvu.”

“Hatupaswi kukubali kuharibiwa umoja wetu. Tunapaswa kufanya kazi pamoja ili kulinda amani na kutatua tofauti zetu kwa njia ya mazungumzo na kuelewana. Umoja wetu ni msingi wa nguvu na amani,” amesema Balozi Dkt. Nchimbi.

Balozi Nchimbi ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa eneo la Tinde mkoani Shinyanga, ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ndani ya mkoa huo, akiongozana na Katibu wa NEC-Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu Amos Makalla pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndugu Rabia Abdalla Hamid

Post a Comment

0 Comments