Ticker

6/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI KIRUSWA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA UCHAGUZI WA VIONGOZI FEMATA

Na Hamida Kamchalla, TANGA.

NAIBU Waziri wa Madini, Steven Kiruswa amefungua mkutano mkuu wa uchaguzi wa viongozi Shirikisho la Vyama vya Wachimba Madini Tanzania (FEMATA) uliofanyika leo Octoba 10, jijini Tanga.

Kiruswa amewataka wajumbe kufanya uchaguzi kwa kufuatia katiba ya shirikisho lao huku akibainisha kuwa serikali imetatua na itaendelea kutatua kero za wachimbaji wa madini na iuwataka viongozi watakaochaguliwa kuandaa mkutano wa kutoa majibu ya kero zao.

"Rais nitoe agizo kwa uongozi unaochaguliwa leo, awe wewe au yeyote atakayekalia kitu hiki, baada ya uchaguzi kuisha salama, atuandalie mkutano ambao utatupa majibu ya maswali na kero zenu zote mlizowasilisha hapa,

"Kwa maana majibu yake nasubiri muda ufike kuyapitisha lakini kwa yale yatakayokosa majibu, serikali yenu ni sikivu itaendelea kuyafanyia kazi" amesema.

Akiongea kabla ya uchaguzi huo, Rais anayemaliza muda wake John Wambura amesema kwamba serikali inaendelea kutatua kero za wachimbaji wa madini na kuagiza uongozi utakaochaguliwa utatoa majibu baada ya uchaguzi.

Wambura ambaye pia anagombea na kutetea kiti chake amebainisha kwamba katika kipindi chake maendeleo makubwa yamepatikana ikiwemo ukuaji wa sekta hiyo na kuongeza mapato kwa wachimbaji wadogo.

"Lakini wakati naingia madarakani kulikuwa hakuna soko la madini, lakini nimeishauri serikali kupitia shirikisho na soko limeoatikana pia kulikuwa hakuna mahusiano mahususi na ya karibu kati ya serikali na wachimbaji, hili limefanyika,

"Na ndiyo maana unaona kila tukiita mikutano ya wachimbaji madini Tanzania, viongozi wetu wanatamani kufika, lakini kipimo tosha ni mkutano huu wa leo, tulialika na tunategemea watafika hapa asilimia 100 na mpaka sasa wamefika asilimia 98, hii inaonesha ni jinsi gani FEMATA wanafanya vizuri" amebainisha.

Post a Comment

0 Comments