Ticker

6/recent/ticker-posts

MKUU WA MISHENI YA UANGALIZI WA UCHAGUZI YA SADC NCHINI MSUMBIJI AFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA VYAMA VYA UPINZANI VYA NCHINI MSUMBIJI

Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC –SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume tarehe 06 Oktoba, 2024 jijini Maputo amefanya mazungumzo na viongozi na wawakilishi kadhaa wa vyama vya upinzani vya Msumbiji ikiwa ni mwendelezo wa jukumu lake la kukutana na wadau mbalimbali wa uchaguzi mkuu wa Msumbiji unaotarajiwa kufanyika tarehe 09 Oktoba 2024.

Katika mazungumzo yake na viongozi hao kutoka vyama vya MPD, PEMO, UDM, RD, PDM, Ecologists na PPD, Mhe. Dkt. Karume pamoja na mambo mengine aliwaeleza lengo la Misheni anayoiongoza kuwa ni kuangalia uchaguzi kwa mujibu wa kanuni na miongozo ya uchaguzi ya SADC iliyorekebishwa mwaka 2021 inayozingatia misingi ya haki, usawa na demokrasia. Pia alitumia fursa hiyo kuwatakia wananchi wa Msumbiji uchaguzi wa amani na utulivu.

Ujumbe wa Mhe. Dkt. Karume kwenye mkutano huo uliwajumuisha Wajumbe wa Troika kutoka Tanzania, Zambia na Malawi, Sekretarieti ya SADC akiwemo Mkurugenzi wa Organ , Prof. Kula Ishmael Theletsane na Wajumbe wa Baraza la Ushauri wa masuala ya Uchaguzi la SADC (SEAC). Wajumbe wa Troika kutoka Tanzania walioshiriki ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiriano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaibu Mussa na Mshauri wa Rais masuala ya Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Sofia Mjema.

Mhe. Dkt. Karume kwa nafasi yake ya Mkuu wa Uangalizi wa Uchaguzi ya SADC ameendelea kukutana na viongozi wa Serikali na wadau mbalimbali wa uchaguzi ambapo hadi sasa amekutana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Msumbiji (CNE), Mabalozi wa Nchi za SADC waliopo Msumbiji, Waziri wa Mambo ya Nje wa Msumbiji, Kamishna Msidizi wa Jeshi la Polisi la Msumbiji na Mgombea urais wa Chama Tawala cha FRELIMO, Mhe. Daniel Francisco Chapo na Viongozi wa dini.
Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC –SEOM) nchini Msumbiji, Mhe. Dkt. Amani Abeid Karume akizungumza na viongozi kadhaa wa vyama vya upinzani vya Msumbiji ikiwa ni mwendelezo wa jukumu lake la kukutana na wadau mbalimbali wa uchaguzi mkuu wa Msumbiji unaotarajiwa kufanyika tarehe 09 Oktoba 2024. Mkutano huo umefanyika tarehe 06 Oktoba 2024 jijini Maputo na kuwahusisha viongozi kutoka vyama vya MPD, PEMO, UDM, RD, PDM na PPD.
Mjumbe wa Troika kutoka Tanzania ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaibu Mussa akijitambulisha wakati wa kikao kati ya Mkuu wa Misheni ya Uangalizi ya SADC, Mhe. Dkt. Karume na viongozi wa vyama vya upinzani vya nchini Msumbiji.
Mjumbe wa Troika kutoka Tanzania ambaye pia ni Mshauri wa Rais masuala ya Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Sofia Mjema akijitambulisha wakati wa kikao kati ya Mkuu wa Misheni ya Uangalizi ya SADC, Mhe. Dkt. Karume na viongozi wa vyama vya upinzani vya nchini Msumbiji.
Sehemu ya viongozi hao wa vyama vya upinzani vya Msumbiji wakizungumza wakati wa kikao kati yao na Mkuu wa Misheni ya SADC ya Uangalizi wa Uchaguzi nchini humo, Mhe. Dkt. Karume

Kiongozi wa Chama cha Ecologists akizungumza

Kikao kikiendelea
Kikao kikiendelea
Kikao kikiendelea
Mjumbe kutoka Baraza la SADC la Ushauri kuhusu masuala ya Uchaguzi akizungumza

Mjumbe wa Troika kutoka Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Talha Waziri akizungumza

Mhe. Dkt. Karume akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya viongozi wa vyama vya upinzani aliokutana nao

Picha ya pamoja

Picha ya pamoja

Picha ya pamoja
Picha ya pamoja.

Post a Comment

0 Comments