Ticker

6/recent/ticker-posts

MABORESHO BANDARI YA TANGA, UFANISI NA MAPATO VYAONGEZEKA


Na Hamida Kamchalla TANGA.

KUFUATIA maboresho makubwa bandari ya Tanga, meli nyingine kubwa ya Kampuni ya Seafront Shipping Ltd iliyobeba shehena yenye bidhaa mchanganyiko yakiwemo magari makubwa ya mizigozaidi ya 300 imetia nanga bandarini hapo.

Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA), Enock Bwigane ameyasema hayo bandarini hapo wakati wa upakuaji wa bidhaa hizo ambazo kiasi kubwa zinapelekwa nje ya nchi.

Bwigane amesema Kampuni hiyo ni mteja mkubwa ambayo unafanya kazi za kibandari katika bandari ya Dar es salaam na tangu imeanza kupitisha mizigo bandari ya Tanga hii ni mara ya 12.

"Uwekezaji uliofanywa na serikali wa sh bilioni 429.1, kuboresha bandari ya Tanga umepelekea sasa meli kubwa, nyingi na kwa shehena tofauti kuhusumiwa katika bandari hii, huyu ni mteja mmoja wapo anayeleta mizigo kutoka nchini Chini" amesema.

Pia kufuatia maboresho hayo, mapato yameongezeka na kuanzia julai 1, hadi Septemba 30 mwaka huu, makusanyo ni sh bilioni 18.6 na katika ya hizo sh bilioni 8 zimetokana na Kampuni Sea Front.

Bwigane amebainisha ufanisi, mapato na shehena vinaongezeka kila mwaka ambapo miaka miwili iliyopita shehena tani laki 8 zilihudumiwa na sasa zimefikia tani milioni 1.1, huku wakitegemea tani milioni 1.4 mwaka huu.

"Katika robo tatu ya kwanza mwaka huu tayari tumesha hudumia tani laki 3.3, kwahiyo tunapiga hatua kubwa katika kuhusumiwa shehena nyingi kwa Mkoa lakini pia katika ushoroba wa Kaskazini' amesema.

Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Mrisha amesema kufuatia uborwshaji huo ajira nyinga kwa vijana zimeongezeka kupitia ongezeko la makampuni ambayo yamesajiliwa kufanya kazi na bandari hiyo.

Amesema awali kabla ya maboresho yalikuwepo makampuni 32 pekee yaliyosajiliwa lakini kwasasa yamesajiliwa mengine 132 na kufanya idadi kubwa ya ajira kuongezeka.

"Awali tulikuwa tunafanya kazi na makampuni ya clearing agent 32 na baada ya maboresho, mpaka kufikia wiki iliyopita tumeweza kusajili makampuni mengine 132 hivyo tuna jumla ya makampuni 164" amebainisha Mrisha.

Naye Ofisa Mwandamizi wa Utekelezaji Bandari ya Tanga, Mussa Mrindoko amesema meli ya Zing Hai Rong 15, Kampuni ya Seafront Shipping imebeba magari 168 yanayoshwa ndani ya nchi na 157 yanakwenda nje ya nchi.

Mbali na magari pia kuna shehena ya mabomba, vifaa na malighafi vya ujenzi, mifuko ya Aluminium kwa ajili ya kutengenezea sabuni, na mizigo hiyo itahudumiwa ndani ya saa 48 kwa awamu 6, kwa maana ya awamu 3 ndani ya saa 24.

"Meli inapokuja kushusha mizigo tunahudumia wateja wetu wote kuanzia wale wanaokuja na meli pamoja na wale wanaopakua mizigo kwenda maeneo mbalimbali ya ndani n nje ya nchi" amefafanua.

Post a Comment

0 Comments