Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amewasili na kupokelewa rasmi Mkoa wa Shinyanga, leo tarehe 9 Oktoba 2024, tayari kuanza ziara ya siku tatu katika maeneo mbalimbali ya wilaya za mkoa huo.
Balozi Nchimbi ambaye ameambatana na Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Amos Gabriel Makalla na Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (Suki), Ndugu Rabia Hamid Abdalla, ameingia Shinyanga akitokea Mkoa wa Simiyu, ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020 - 2025, kusikiliza kero na changamoto za wananchi kisha kuzitafutia majawabu na kuhamasisha uimara wa CCM kuanzia ngazi ya mashina.
0 Comments