Ticker

6/recent/ticker-posts

KATIBU MTENDAJI BMT AWAFUNDA VIONGOZI WA SHIMUTA


KATIBU Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Neema Msitha akizungumza wakati akifunga mafunzo ya ya Saikolojia na Uongozi Michezoni Jijini Tanga
KATIBU Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Neema Msitha kushoto akimkabidhi cheti cha ushiriki wa mafunzo hayo Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Shimuta na Mwenyekiti wa Michezo kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Elinaike Nabur
KATIBU Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Neema Msitha kushoto akimkabidhi cheti cha ushiriki wa mafunzo hayo Mwenyekiti wa Michezo kutoka TFS na Mjumbe wa Kamati ya Fedha ya Shimuta Marcel Bitulo

Na Oscar Assenga, TANGA.

KATIBU Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Neema Msitha amelitaka Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma,Taasisi na Makampuni Binafsi (SHIMUTA) kutengeneza kanuni na miongozi mizuri ili kuondoa migogoro wakati wa Mashindano kuachana na Mamluki na makandokando ya kubadilisha ratiba mara kwa mara.

Neema aliyasema hayo Jijini Tanga wakati akifunga mafunzo ya Saikolojia na Uongozi Michezoni Jijini Tanga ambapo alisema hawatarajii kuona mambo kama hayo yanajitokeza kwenye mashindano hayo badala yake muhimu wakazingatia kanuni na miongozo.

Alisema pia uwepo wa kanuni na miongozo imara itasaidia kuwaepusha na mitafaruku ambayo haina tija wakati wa mashindano na kushindwa kufikia malengo ambayo wamejiwekea

“Hatutarajii kukutana na mambo hayo tuzingatie kanuni na miongozi tuliojiwekea na matarajio yetu ni kuona Shimuta inakuwa na matarajio makubwa ya kuacha alama kwenye mashindano hatuwezi kupeleka malalamikio hayo mbele ya kwa viongozi”Alisema

Katibu huyo alisema kwamba wanatarajia kuona shirikisho hilo kinakuwa na mipango mikubwa ikiwemo kuona namna ya kununua eneo Tanga kwa ajili ya kujenga kituo cha Mashindano wakiwa kazini watoto watacheza pale.

“Lakini pia tunatarajia kuona kama Shimuta mwaka ujao tunachanisha watu fedha zitakazoptikana tutanunua mipira na kupeleka kwenye shule 56 za michezo zilizoteuliwa na Serikali na mambo mengine ya kimaendeleo na sio suala la mamluki”Alisema

Hata hivyo aliwataka watumishi kuwa na mahusiano mazuri na waajiri vizuri katika kutetea suala la Shimuta na wasiende kugeuka kuwa kero kwao.

“Niwapongeza viongozi wa shimuta kwa kuweza kubuni na kufanya vitu ambavyo vitasaidia kuleta maendeleo kwenye michezo yao mahali pa kazi tunafahamu kwamba nini katiba yenu inaeleza majukumu yenu tunapaswa kuyafanya”Alisema

Alisema lakini mashirikisho mengi wamekuwa wakijipanga kwa kufikiria mashindano na ndio maana kwenye kufanya mashindano mambo mengi hayaendi sawa kutokana na kwamba kuna masuala wanakuwa hawajapata uelewa nayo ndio maana mkagundua ipo haja ya kufa ya mafunzo hayo.

Alitoa wito kwa washiriki mafunzo hyo kuzingatia walichofundishwea ili wanapokwenda kwenye kazi waweze kuongeza thamani ya uwepo wao kwenye mafunzo hayo huku akieleza kwamba kila mtu anaweza kucheza na sio kusimamia michezo.

“Mafunzo mliyoyapa hapa yakawe chachu na mjitofautishe na wale ambao hawajahudhuria lakini uhai wa binadamu upo kwenye michezo na ndio maana wanawake ukienda hospitalini ukiwa mjamzito unaulizwa mtoto amecheza tumboni michezo ndio kiini cha uhai wa binadamu “Alisema

Aliongeza kwamba sasa kiini hicho watu wanakichukulia rahisi kwamba kila mtu anaweza kuisimamia bila kutambua kwamba ili uweze kusimamia lazima upewa mafunzo kwani michezo ni utaalamu kama ilivyo utaalamu mwengine wowote

“Naomba tukazingitie mafunzo tulioyapata Mahali pa kazi ni kituo kilicholetwa kama ziara kusaidiaa watumishi afya, kutengeneza connection na tuzingatie yale tuliofundishwa tuzingatia maadili ya kazi tunapokuwa kwenye sehemu ya michez ili kutowapa sababu ya watu wanaopiga vita michezo kupata vya kuongea”Alisema

“Lakini wakati wa mashindano Shimuta tumekuwa tukipokea malalamiko mengi kwamba mara ratiba,mamluki,wakijua dhumuni la kuanzishwa Shimuta hawataleta mamluki,kwanini tunawabania watumishi wenzetu na kuwaleta watu ambao sio watumishi na kusababisha uvunjifu wa tabia hivyo nataka tuachana na hilo”Alisema

Awali akizungumza Mwenyekiti wa Shimuta Roselyn Masambu alisema lengo la mafunzo hayo ni muhimu kwa viongozi wa michezo ambao wanaongoza wafanyakazi katika taasisi zao na hivyo wanaamini yatakuwa chachu kubwa kwa maandalizi ya michuano hiyo msimu huu lakini pia kuwa chachu katika michezo kwenye maeneo yao .

Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa Michezo kutoka TFS na Mjumbe wa Kamati ya Fedha ya Shimuta Marcel Bitulo alisema kwamba kwa kutambua sera ya nchi ambayo inataka kila taasisi kutenga bejeti ya michezo kama unavyotambua ili uweze kuwa na tija kwa wafanyakazi lazima utoa kipaumbela suala la michezo na wao wanatambua na wamekuwa wakilifanya mara kwa mara.

Hata hivyo kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Shimuta na Mwenyekiti wa Michezo kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Elinaike Nabur alisema michezo ni sehemu muhimu kwa watumishi ambao muda mwingi wanatumia mahali pa kazi kuhakikisha wanasaidia serikali kufikia jamii kutimiza malengo yao iliyokusudia katika nchi.

Post a Comment

0 Comments