Afisa Mkuu wa Biashara Isack Nchunda ( Kushoto ) , Mkurugenzi wa Masoko Edwardina Mgendi (kulia ), pamoja na wateja wa Tigo kwa miaka 30, wakifungua rasmi Wiki ya Huduma kwa Wateja 2024 kwa kukata utepe maalum, Wiki ambayo Tigo inaungana na Watanzania kusheherekea kufikisha miongo mitatu , huku ikijivunia kutoa huduma bora zaidi kote nchini .
Na Adery Masta.
Kampuni namba moja nchini kwa utoaji wa Huduma za Kidigitali ya Tigo , Leo Oktoba , 07 , 2024 imefungua rasmi sherehe za WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA kwa mwaka 2024 , huku ikijivunia kutoa huduma bora na zilizotukuka kwa watanzania kwa Miaka 30 sasa . Tigo wanasheherekea wiki hii wakiwa na Kaulimbiu , "Above and Beyond" au "Huduma Bora na Zaidi," .
Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa sherehe hizo Bwn. Isack Nchunda, Afisa Mkuu wa Biashara kutoka Tigo amesema
" Ahadi yetu ni kuhakikisha tunatoa huduma bora, za kibunifu, na kwa gharama nafuu kwa wateja wetu. Hatutoi tu bidhaa bora, lakini pia tunajitahidi kuhudumia wateja wetu kwa namna ya kipekee. Timu yetu inahakikisha unapata thamani zaidi, kutoka kwenye huduma zetu za kama simu za mikopo kwa shilingi 650 kwa siku, hadi vifurushi vya saizi yako vinavyokidhi mahitaji yako.
Tumewekeza katika mtandao wa 4G ulioenea kote nchini, 5G yenye kasi zaidi, pamoja na huduma za Fiber zinazokupa intaneti isiyo na kikomo. Huduma zote hizi zimeboreshwa ili kuhakikisha wewe mteja unapata uzoefu bora zaidi.
Tunapoadhimisha miaka 30 ya Tigo, tunatoa shukrani kwa wateja wetu kwa uaminifu wenu. Ninyi ndio sababu ya mafanikio yetu, na tunaendelea kuboresha huduma kila siku kwa ajili yenu.
Heri ya Wiki ya Huduma kwa Wateja!
"Above and Beyond." amesema
Naye Bi. Edwardina Mgendi Mkurugenzi wa Masoko kutoka Tigo ameongezea kwamba
" Wiki ya Huduma kwa Wateja mwaka huu imejikita kuonyesha dhamira yetu ya kuwapa wateja wetu uzoefu wa kipekee katika kila hatua ya safari yao na Tigo, katika kitengo cha Masoko, kazi yetu ni kuhakikisha kila bidhaa na huduma tunayokuletea inakidhi mahitaji yako ya kila siku, kwa ubunifu na ubora usio na kifani.
Huduma zetu zinafikia viwango vya juu kwa wateja wetu – kutoka vifurushi vya simu vilivyobuniwa kwa ajili ya kila aina ya mtumiaji.
Tunafuraha kuwa mstari wa mbele katika kukuletea huduma zinazoendana na maisha yako, tukizingatia kila maoni na hitaji unalotoa.
Uaminifu na imani yako kwetu ni nguzo ya mafanikio yetu, na tutaendelea kujituma zaidi na zaidi ili kuhakikisha unapata huduma bora, kila siku.
Tunaposherehekea miaka 30 ya mafanikio, tunakushukuru kwa kuwa sehemu ya familia ya Tigo. Hatutaacha kwenda "Above and Beyond" kwa ajili yako! "
0 Comments