Na Oscar Assenga,
TANGAMAAMUZI ya Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo wilaya ya Handeni Mkoani Tanga Kombo Mbwana Twaha kupelekwa mahakamani Kuu kwa ajili ya kupewa haki zake ama la itabainika Octoba 31 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama baada ya shauri hilo kuhairishwa Wakili wa Upande wa Utetezi Paul Kisabo alisema kwamba wanaamini mahakama itatenda haki na kutafsiri sheria kama ilivyo watasikia na kukiwa na maamuzi tofauti sheria zitawaelekeza nini cha kufanya .
Shauri hilo lililetwa mahakamani hapo na lilipangwa kwa ajili ya kusikilizwa mbele ya Mhe.Jaji Happiness Ndesamburo ambapo kesi hiyo msingi wake waliifungua kwa ajili ya kuomba Kombo Mbwana Twaha aweze kupelekwa mahakamani ili aweze kupewa haki zake.
Aidha alisema kwamba Kombo anashikiliwa tokea 15 June 2024 alipokamatwa nyumbani kwake Handeni na mpaka leo bado anashikiliwa.
Alisema kesi hiyo msingi wake waliifungua kwa ajili ya kuomba kombo apelekwe mahakamni ili aweze kupewe haki zake kupitia maombi ya kuiomba mahakama kuu itoe amri mtu aletwe Yule aliyeshikiliwa kunyume cha sheria.
Wakili huyo alisema kwamba walifungua kesi hiyo na ilipangwa kusikiliza pande zote mbili wao upande wa mleta maombi Kombo Twaha Mbwana alikuwepo yeye na upande wa wajibu maombi ambaye ni kamansa wa RPC ,IGP,DPP na Mwanasheria Mkuu wa Serikali waliwakilishwana mawakili wawili waliwasilisha hoja zao mahakamani hapo.
Awali akizungumza Katibu wa Chadema wilaya ya Tanga Shabani Ngozi alisema kwamba wamekuja Mahakam kuu kusikiliza kesi hiyo kwa mwenendo wa kesi wanawashukuru mawakili wao kwa kazi kubwa na ngumu wanayoendelea kuifanya kuhakikisha Kombo anapata haki yake ya msingi awe nje kwa dhamana .
Alisema kwa hiyo binafsi wanaendelea kushirikiana na mawakili wao na familia ili mwenzao awe huru waweze kuendeleza gurudumu la kuendeleza Taifa.
0 Comments