Ticker

6/recent/ticker-posts

BENKI YA CRDB YAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA CRDB ...ATM YA KIPEKEE KUWEKA FEDHA SAA 24

   

Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizindua Wiki ya Huduma kwa wateja CRDB Kahama sambamba na ATM ya Kuweka Fedha 
Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi imezindua Wiki ya Huduma kwa Wateja na ATM mpya na ya kipekee ya kuweka fedha ya benki ya CRDB tawi la Kahama ambayo itawawezesha wafanyabiashara na watu wote Kahama kuweka fedha masaa 24.


Uzinduzi huo umefanyika leo Jumatatu Oktoba 7,2024 katika Benki ya CRDB Tawi la Kahama ambapo 
mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga  Mhe. Mboni Mhita.

Akizungumza na Uongozi wa Benki hiyo na wateja wao wakati wa  Uzinduzi wa Wiki ya huduma kwa wateja na ATM Mpya ya kuweka Fedha, Mhe. Mboni  amesema Benki ya CRDB ameipongeza kwa kuweka ATM ya kuweka fedha na kuongeza kuwa benki hiyo ina jukumu la kuhakikisha huduma za kifedha zinawafikia ananchi wengi ili kuwakwamua katika mnyororo wa kiuchumi ikiwemo eneo la biashara, kilimo, n.k.


 Kaimu Meneja CRDB Kanda ya Magharibi Anselm Mwenda amesema Wiki ya huduma kwa wateja ni ishara ya Taasisi hiyo kutambua mchango wa wateja ambao wamekuwa wadau namba moja wa Benki ya CRDB.

Anselm amesema Uzinduzi wa Wiki ya huduma kwa wateja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi umekwenda sambamba na uzinduzi wa huduma mpya ikiwemo ATM ya kuweka fedha katika Tawi la Kahama na ya kipekee Kanda ya Ziwa, lakini pia huduma ya AI Chart Bolt yenye lengo la kuwahudumia kifedha wateja wao kwa njia ya Tovuti na Mtandao wa WhatsApp.

Akizungumza kwa niaba ya Wateja, Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Wilaya ya Kahama na Mteja wa CRDB Charles Machali amewahimiza Wafanyabisahara kutumia huduma za kifedha kutoka Benki hiyo na kuiomba CRDB kuongeza wigo wa kuwafikia zaidi Waananchi kwa huduma za kifedha.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akiweka Fedha kwenye ATM mpya ya kuweka fedha ya benki ya CRDB tawi la Kahama. ATM hii itawawezesha wafanyabiashara na watu wote Kahama kuweka fedha masaa 24
Kaimu Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Anselm Mwenda akiongea wakati wa uzinduzi

Post a Comment

0 Comments