Ticker

6/recent/ticker-posts

AKIBA COMMERCIAL BANK PLC YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

  

Mkurugenzi Mtendaji wa Akiba Commercial Bank Plc, Bw: Silvest Arumasi akitoa hati ya shukrani kwa Bi. Twaiba Msechu wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja katika tawi la Ubungo


Na Mwandishi wetu  Dar es salaam

  Akiba Commercial Bank Plc  imewashukuru wateja wake  kuungana nao katika safari hii ya kutoa huduma bora zaidi za kibenki ambazo zinachangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa Watanzania.

Shukrani hizo zimetolewa  leo Octoba 9,2024 Dar es salaam na  Mkurugenzi Mtendaji waIBA benki ya Akiba Commercia Bw Silvest Arumasi katika  Maadhimisho ya Wiki ya huduma  kwa wateja hafla iliyofanyika   tawi la  Ubungo la benki hiyo  na kuhudhuriwa na Wateja  wafanyakazi wa benki , na wawakilishi wa vyombo vya habari.

Mkurugenzi amesema wiki ya huduma kwa wateja  wameifanya kwa namna ya kipekee kwa  kutambua thamani ya wateja kwa kutoa tunzo kwani kufanya hivyo ni  kuonesha ahadi ya benki ya kuendelea kutoa huduma bora.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “Above and Beyond” ikimaanisha kwenda zaidi ya matarajio, kauli ambayo inakusudia kuhamasisha utoaji wa huduma bora zaidi kwa wateja.

“Niwashukuru wateja wetu kutuchagua kuwa washirika wenu wa kibiashara kwani bila nyinyi , tusingeweza kufikia mafanikio haya tunayojivunia leo hivyo wiki hii ni maalum kwa ajili yenu, tunathamini na  kutambua mchango wenu ” amesema  Arumasi

 Hata hivyo Akiba Commercial  benki imefanya maboresho yaliyofanyika katika huduma za kidijitali za benki, ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma za ACB Mobile na Akiba Wakala kwa kuzingatia mahitaji ya wateja. 


 Akiba Commercial benki inafanya   huduma mpya ya Internet Banking inayopatikana kwa wateja binafsi, makampuni makubwa, na taasisi mbalimbali, kama sehemu ya mkakati wa mabadiliko ya kidijitali wa benki hiyo kwa kauli mbiu “Twende Kidijitali.”“Kwa kuzingatia mabadiliko ya haraka ya kiteknolojia.

 " Mwaka 2024 tumeamua kuupa  jina la Mwaka wa Kidijitali,’ na tumejidhatiti kuwafikishia huduma za kibenki kwa njia ya kisasa zaidi kupitia mifumo yetu ya kidijitali,” aliongeza Bw. Arumasi.

Maadhimisho ya  wiki ya huduma kwa wateja, Akiba Commercial Bank inafanya shughuli mbalimbali katika matawi yake yaliyopo Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Moshi, Mbeya, na Dodoma ili kuwapa wateja fursa ya kuona na kushiriki katika maboresho yanayoendelea kufanywa.

 Aidha Benki itaendelea  kukusanya  maoni na mapendekezo kutoka kwa wateja ili kuboresha bidhaa na huduma zake kwa ujumla.“Wiki hii siyo tu kwa ajili ya sherehe, bali ni ahadi yetu ya kuendelea kuboresha na kutoa huduma bora ambazo zitazidi matarajio yenu,” amesema Bw. Arumasi. “

Post a Comment

0 Comments