Ticker

6/recent/ticker-posts

WANAHARAKATI WAHIMIZA ELIMU KUTOLEWA KUKOMESHA MILA KANDAMIZI

WANAHARAKATI wa Jinsia na Maendeleo wameiomba Serikali pamoja na taasisi mbalimbali kutoa elimu kwa jamii ili kufanya mageuzi na kuachana na mila kandamizi ambazo zimekuwa zikimnyanyasa mwanamke.

Ombi hilo wamelitoa leo Septemba 25,2024, katika viunga vya mtandao wa Jinsia Tanzania Mabibo-Jijini Dar es Salaam,wakati wakijadili mada isemayo "Je!Ni kwa namna gani Mila na Tamaduni zinawakandamiza wanawake katika jamii?".

Aidha wanaharakati hao wa masuala ya Jinsia wamebainisha kuwa mila na tamaduni nyingi zinamnyima mwanamke nafasi ya kurithi mali jambo ambalo limekuwa likichochea kuachwa nyuma kwa kundi hilo.

Wameeleza kuwa ndoa za utotoni pamoja na ukosefu wa elimu kwa kundi kubwa la watu ni sababu kubwa ambazo zinachangia kukandamizwa kwa Jinsia moja pekee ambapo mtoto wa kike hapewi kipaumbele katika urithi wa mali kwa kigezo cha kuolewa.

Vile vile wanaharakati wamesema kuwa, kutelekezewa mzigo wa majukumu ya familia,pamoja na kukosa nafasi katika ngazi za uongozi ni mambo ambayo yanaendelea kumdidimiza mwanamke na kuendelea kumfanya kuwa tegemezi.

Aidha Wadau hao wa semina za Jinsia na Maendeleo,wametoa mapendekezo yao ambapo wamesema mitaala ya elimu iboreshwe pamoja na kufanya ushirikishwaji kwa wazee wa mila na serikali kukaa pamoja na kuorodhesha mila kandamizi ili kuzikomesha.

Post a Comment

0 Comments