Ticker

6/recent/ticker-posts

RC MACHA AHAMASISHA WANANCHI KUJISAJILI NA KUSHIRIKI SHYCOM ALUMNI MARATHON 2024


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha (kushoto) akijisajili kushiriki Mbio za Shycom Alumni Marathon zitakazofanyika Septemba 21,2024 katika Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha (katikati) akijisajili kushiriki Mbio za Shycom Alumni Marathon zitakazofanyika Septemba 21,2024 katika Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akionesha namna ya kujisajili kushiriki Mbio za Shycom Alumni Marathon zitakazofanyika Septemba 21,2024 katika Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

***

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha ametoa wito kwa wananchi wote kujitokeza, kujisajili ili waweze kushiriki vema katika tukio muhimu la mbio za Shycom Alumni Marathon litakalofanyika tarehe 21 Septemba, 2024 lenye lengo kuu la kuchangia fedha zitakazoboresha miundombinu ya Chuo cha Ualimu Shinyanga maarufu 'Shycom' kilichopo Mjini Shinyanga.

Mhe. Macha ameyasema haya leo Septemba 14, 2024 ofisini kwake alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa tukio hili ambapo amesema mbio hizo zitawezesha kuimarisha uhusiano, kuboresha afya, kutambua na kujenga vipaji, kuchangia damu na kwamba takribani washiriki 1000 wanatarajiwa katika tukio hili.

“Nawapongeza sana kwa kuanzisha mbio hizi za Shycom Alumni Marathon na mimi nitashiriki mbio hizi na tayari nimeshajisajili na nimelipia pesa,”amesema Macha.

"Naomba kutoa wito kwa wananchi wote kujitokeza, kujiandikisha na kushiriki kikamilifu katika mbio hizi za hisani zilizopewa jina Shycom Alumni Marathon ili tuweze kutimiza lengo la kuchangia fedha kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya chuo, kuimarisha umoja, uhusiano wetu, kuboresha afya zetu, kubainisha na kujenga vipaji kwa vijana wetu na kuchangia damu itakayowasaidia wagonjwa katika vituo vyetu vya afya," ameongeza Macha.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha 

Ameeleza kuwa, Serikali ya Mkoa wa Shinyanga imewahakikishia usalama wakati wote wanamichezo wote watakaofika mkoani Shinyanga na kushiriki katika Shycom Alumni Marathon huku akiwasihi wafanyabiashara kutumia vema fursa ya uwepo wa mbio hizi kwani watu 1000 siyo wachache.

Katika hatua nyingine ametoa wito pia kwa watu na viongozi, kwamba katika shule zao walizosoma watafutane na kuungana kwa pamoja, ili wajadili namna ya kukarabati shule ambazo walisoma, kwa kuboresha miundombinu ya shule.
Anorld Bweichum

Mratibu wa Mbio za Shycom Alumni Marathon Anorld Bweichum, amesema maandalizi ya mbio hizo yameshakamilika kwa asilimia 90 na wananchi ambao watashiriki mbio hizo wanapaswa kulipia kiasi cha fedha sh.35,000 ili kujisajili na mgeni rasmi siku hiyo atakuwa Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda.

Naye mmoja wa ambao wamewahi kusoma katika chuo hicho Robert Kazinza amesema wameanzisha wazo hilo ili kupata fedha za kuboresha miundombinu ya chuo cha Shycom.

Mwakilishi wa Mkuu wa chuo cha Shycom Shinje Charles, amesema fedha zitazopatikana zitatumika kukarabati mabweni, madarasa, mfumo wa majitaka, na miundombinu mingine ili kuweka mazingira mazuri ya wanafunzi kusoma.

Shycom Alumni Marathoni ni mbio za hisani ambazo zimeandaliwa kwa maalum kwa waliosoma au kupita Shycom tangu kuanzishwa kwake mwaka 1965 wakiwemo waliokuwa Wadhibiti na Wakaguzi Wakuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kama vile Charles Kichere na ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Elimu Mhe. Adolf Mkenda (MB) sanjari na mwenyeji wake Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha.

                                              ***
Karibu kushiriki Mbio za Shycom Alumni Marathon tarehe 21 Septemba katika Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga. Gharama za Ushiriki wa Mbio ni TZS 35,000 tu kwa mbio za KM 5, KM 10 na KM 21. Kwa mawasiliano zaidi, piga 0756254146. Jisajili Sasa!"

Unaweza kufanya Malipo ya Shycom Alumni Marathon Kwa Shilingi 35,000 Kila Mshiriki Atapata T-shirt na Medali. Ili kufanya Malipo Kwa Kutumia laini ya Tigo Pesa Fuata Hatua zifuatazo: 

- Piga *150*01# 
- Chagua No 5 (Lipa Kwa Simu) 
- Chagua 6 (Tickets)
- Chagua 1 (Marathon) 
- Chagua 5 (Endelea) 
- Chagua No 1 (Shycom Alumni Marathon) 
- Fuata Maelekezo zaidi. 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza kuhusu Mbio za Shycom Alumni Marathon zitakazofanyika Septemba 21,2024 katika Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha (katikati) akijisajili kushiriki Mbio za Shycom Alumni Marathon zitakazofanyika Septemba 21,2024 katika Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.

Post a Comment

0 Comments