Ticker

6/recent/ticker-posts

KAMPUNI YA BAKHRESA YAGAWA MAJIKO YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KWA BABA NA MAMA LISHE KISUTU

NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV 

KAMPUNI ya Bakhresa Group kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa (UNIDO) wamekabidhi majiko ya gesi 60 kwa mama na baba lishe wa soko la Kisutu  ili kuhakikisha wanaacha kutumia nishati chafu ya kupikia.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 27,2024 Jijini Dar es Salaam kwenye zoezi la ugawaji wa majiko hayo, Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Christina Mndeme amesema kitendo walichokifanya kampuni ya Azam ni kuunga mkono jitihada za serikali kuhakikisha inakomesha matumizi ya nishati chafu.

Aidha Bi.Christina Mndeme ametoa Rai kwa sekta nyingine. binafsi kuunga mkono Juhudi zinazofanyika ili kuongeza nguvu katika kampeni ya nishati safi ya kupikia ambapo itasaidia kufikia lengo kabla hata ya muda uliokusudiwa.

"Tukiunganisha nguvu kwa pamoja,  inawezekana kabla hata ya 2034 asilimia 80 ya watanzania ikafikiwa ambayo itakuwa unatumia nishati safi ya kupikia"Amesema

Pamoja na hayo Mndeme ameeleza kuwa majiko hayo waliyoyatoa yametengenezwa na kampuni ya MOTO POA yanatumia teknolojia ya gesi ya Ethanal ambayo inapatikana baada ya mchakato wa kuzalisha sukari ambapo inasaidia kupunguza athari ya gesi joto angani.

Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Bakhresa Group,Rehema Salim amesema wanatarajia kuendelea kutoa majiko hayo katika maeneo mengine nchini ambapo leo wamefanikiwa kutoa majiko 60;kwa mkoa wa Dar es Salaam ambapo lengo lao nikutoa majiko 500 kwa mkoa huo.

Aidha Rehema ameeleza kuwa majiko hayo ni mazuri kwani hayatoi Moshi wala hayatoi uchafu na nishati yake inapatikana kwa urahisi nchini kwa gharama nafuu ambayo mwananchi wa kawaida anaweza kuimudu.

Post a Comment

0 Comments