KAMATI
ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imepongeza juhudi za
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika kuboresha mitaala yake ili kukidhi
mahitaji ya soko la ajira.
Hayo
yamebainishwa leo Septemba 10, 2024 Jijini Dar es Salaam na kamati
hiyo wakati ilipofanya ziara kwenye Chuo hicho kukagua utekelezaji wa
Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya kiuchumi (HEET).
Kamati
hiyo ilibaini kwamba hatua hii ya kufanya mapitio ya mitaala imekuwa na
mchango mkubwa katika kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira nchini.
Mwenyekiti
wa Kamati hiyo, Mhe. Husna Sekiboko amesema kwa muda mrefu ajira
imekuwa kilio cha vijana licha ya kusoma elimu ya juu, hivyo tathmini ya
aina hiyo ni muhimu ili kuhakikisha elimu inayotolewa ndiyo inahitajika
kwenye soko la ajira.
"Kilichofanyika
ni kizuri maana tusijifungie kwenye kutoa elimu bila kujifanyia
tathmini kujua elimu inayotolewa inatatua changamoto zinazotuzunguka? Je
mhitimu kwa ngazi ya chuo kikuu ana uwezo wa kutatua changamoto
zilizopo kwenye jamii.
“Tumefurahishwa
pia na taarifa kwamba mnafanya tafiti ila tunachotaka matokeo ya tafiti
hizi yawekewe wazo ili ziwe msaada kwenye jamii isiwe tafiti
zinafanyika na kuishia kwenye makabati," amesema Mhe. Sekiboko.
Kwa
upande wake Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Mipango, Fedha na Utawala, ambaye
pia ni Mratibu wa mradi huo, Prof. Bernadeta Killian amesema tayari
chuo hicho kimefanya mapitio ya mitalaa 60 kwa ngazi ya shahada ya
kwanza na ya pili na iko katika hatua za mwisho kabla ya kuanza
kutumika.
Aidha
amesema utekelezaji wa mradi wa HEET katika Taasisi ya Sayansi za
Bahari, unahusisha ujenzi wa majengo mawili ambayo ni bweni lenye uwezo
wa kuchukua wanafunzi 40 na kukamilisha jengo la utawala na taaluma.
Amesema
jengo la utawala na taaluma litakuwa na madarasa manne yenye uwezo wa
kuchukua jumla ya wanafunzi 216, ukumbi wa mikutano wenye uwezo wa
kuchukua watu 150, ofisi ya wafanyakazi, na maabara tano.
Pamoja
na hayo Prof. Killian amesema ujenzi wa majengo mbalimbali ya mradi
ulianza Februari ,2024 na utakamilika baada ya miezi 18 na utagharimu
kiasi cha Tsh. 11, 194,677,531.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Mhe. Husna Juma Sekiboko akizungumza na wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mara baada ya kufanya ziara kutembelea utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Uchumi (HEET) leo Septemba 10, 2024 katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omary Kipanga akizungumza wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo ilipofanya ziara kukagua utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Uchumi (HEET) katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Septemba 10, 2024.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Mipango, Fedha na Utawala, ambaye pia ni Mratibu wa mradi huo, Prof. Bernadeta Killian akizungumza wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo ilipofanya ziara kukagua utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Uchumi (HEET) katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Septemba 10, 2024.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Mhe. Husna Juma Sekiboko, (mwenye ushungi) akiongozana na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Mipango, Fedha na Utawala, ambaye pia ni Mratibu wa mradi huo, Prof. Bernadeta Killian pamoja na Wajumbe wa Kamati wakati walipofanya ziara katika Taasisi ya Sayansi za Bahari, Buyu visiwani Zanzibar Septemba 9,2024.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Mhe. Husna Juma Sekiboko, (mwenye ushungi) akiongozana na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omary Kipanga, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Mipango, Fedha na Utawala, ambaye pia ni Mratibu wa mradi huo, Prof. Bernadeta Killian pamoja na Wajumbe wa Kamati wakati walipofanya ziara katika Taasisi ya Sayansi za Bahari, Buyu visiwani Zanzibar Septemba 9,2024.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Husna Juma Sekiboko wakikagua mradi wa ujenzi wa jengo la Taaluma na Utawala unaotekelezwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Uchumi (HEET) wakati walipofanya ziara katika Taasisi ya Sayansi za Bahari, Buyu visiwani Zanzibar Septemba 9,2024.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Husna Juma Sekiboko wakikagua mradi wa ujenzi wa jengo la Taaluma na Utawala unaotekelezwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Uchumi (HEET) wakati walipofanya ziara katika Taasisi ya Sayansi za Bahari, Buyu visiwani Zanzibar Septemba 9,2024.
Ujenzi wa engo la Taaluma na Utawala ukiendelea katika Taasisi ya Sayansi za Bahari, Buyu visiwani Zanzibar.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omary Kipanga akizungumza jambo na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Mipango, Fedha na Utawala, ambaye pia ni Mratibu wa mradi huo, Prof. Bernadeta Killian wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Husna Juma Sekiboko kufanya ziara katika Taasisi ya Sayansi za Bahari, Buyu visiwani Zanzibar Septemba 9,2024.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Husna Juma Sekiboko wakikagua mradi wa ujenzi wa bweni unaotekelezwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Uchumi (HEET) wakati walipofanya ziara katika Taasisi ya Sayansi za Bahari, Buyu visiwani Zanzibar Septemba 9,2024.
0 Comments