Ticker

6/recent/ticker-posts

Equity na Bakhresa Washirikiana Kuongeza Mitaji kwa Wafanyabiashara wa Unga

BENKI ya Equity imeingia makubaliano na kampuni ya Bakhresa yenye lengo la kutoa mikopo kwa wafanyabiashara wa unga, ambapo mfanyabiashara atakuwa na uwezo wa kukopa fedha kwa ajili ya kupata bidhaa hiyo mpaka zaidi ya Shilingi Milioni  300.

Akizungumza leo Septemba 26,2024 Jijini Dar es Salaam katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Biashara wa benki ya Equity  Leah Ayoub amesema lengo ni kuhakikisha wafanyabiashara wanakuza mitaji ambapo kama benki  wanatamani wateja hao wakope zaidi ya Sh Milioni 300.

“Tumeingia makubaliano kati ya benki ya Equity na kampuni ya Bakhresa yenye lengo la kutoa mikopo kwa wafanyabiashara wa unga,mfanyabiashara atakuwa na iwezo wakukopa fedha kwa ajili ya kuoata bidhaa hiyo mpaka zaidi ya Shilingi Milioni  300,”amesema.

Amesema mkopo huo hautakuwa na riba isipokuwa mteja atalipa kamisheni yakuanzia asilimia 0.5 mpaka 1.5 ambapo mkopaji  atapaswa kulipa  fedha hizo kuanzia siku saba hadi  30.

“Hii ni  fursa  ya kukuza mtaji wako kwa haraka,tumeamua kujitoa kwa wajasiriamali na kuwawezesha wapate  huduma kwa urahisi bila vikwazo vingi ambapo mteja hata kama hana akaunto ya Equity ana uwezo wakuifungua kiganjanjani mwake akapata mkopo,”amesema Leah.

Naye Mkurugenzi wa Uhusiano wa kampuni Bakhresa Group  Hussein Sufiani amesema makubaliano hayo yatamsaidia mteja ambapo badala kuhangaika kutafuta mfadhili au mdhamini wa kumpatia fedha anaweza kwenda benki au kutumia mtandao kupata huduma.

“Hii nayo ni kidigitali, utapata huduma hiyo kwa mfumo wa sms (ujumbe mfupi), sio lazima  uende benki kufanya transfer (kuhamisha) inafanyika moja kwa  moja ukishafanya oda yako, kadri  unavyozidi kukopa kiwango kinakua,”amesema Sufiani.

Amesema huduma hiyo itawasaidia zaidi  wateja wao hasa wadogo hivyo amewahimiza kuchangamkia  fursa hiyo.

Post a Comment

0 Comments