Ticker

6/recent/ticker-posts

BARRICK YATOA MSAADA WA KOMPYUTA KATIKA SEKONDARI YA WASICHANA KUWAWEZESHA KUPATA ELIMU KIDIGITALI

Mgeni Rasmi kutoka Barrick, Georgia Mutagahywa (kushoto)akionyeshwa ramani ya miundombinu ya shule hiyo
Wanafunzi wakipokea kompyuta zilizotolewa na Barrick
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Wasichana ya Barbro Johansson wakionyesha kompyuta zilizotolewa na kampuni ya Barrick wakati wa mahafali ya kidato cha nne ya shule hiyo
Meneja Mawasiliano wa Barrick nchini (Corporate Communications and Country Liaison Manager), Georgia Mutagahywa, akiongea na wahitimu ,wazazi na wanafunzi katika shule ya sekondari ya Barbro Johansson iliyopo jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa mgeni rasmi na kukabidhi kompyuta 15 za kisasa zilizotolewa na Barrick kwa ajili ya kuimarisha maabara ya kompyuta ya shule hiyo.
Meneja Mawasiliano wa Barrick nchini (Corporate Communications and Country Liaison Manager), Georgia Mutagahywa, akiongea na wahitimu ,wazazi na wanafunzi katika shule ya sekondari ya Barbro Johansson iliyopo jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa mgeni rasmi na kukabidhi kompyuta 15 za kisasa zilizotolewa na Barrick kwa ajili ya kuimarisha maabara ya kompyuta ya shule hiyo.
Mwenyekiti wa taasisi ya Joha Trust na Mwanzilishi wa shule za Wasichana ya Barbro Johansson nchini, Profesa Anna Tibaijuka akiongea katika mahafali hayo
Mmoja wa wahitimu akipokea cheti kutoka kwa mgeni rasmi
Baadhi ya wahitimu katika picha ya pamoja na mgeni rasmi na viongozi wa shule waliokuwa katika meza kuu
Baadhi ya wahitimu wakifuatilia matukio wakati wa mahafali hayo
Awali Mgeni rasmi akiwasili katika mahafali hayo

**

Wanafunzi wanaosoma katika shule ya sekondari ya Wasichana ya Barbro Johansson iliyopo Luguruni jijini Dar es Salaam wametakiwa kuweka bidii kubwa katika masomo yao sambamba na kujiamini na kuwa na nia ya kufuata nyayo za wanawake wanaofanya mambo makubwa katika jamii ili kuhakikisha wanatimiza ndoto zao za baadaye baada ya kumaliza masomo.Wito huu ulitolewa na Meneja Mawasiliano wa Barrick nchini (Corporate Communications and Country Liaison Manager), Georgia Mutagahywa, wakati wa mahafali ya 22 ya kidato cha nne shuleni hapo ambapo alikuwa mgeni rasmi.

Katika mwendelezo wa kuunga mkono kufanikisha elimu kwa watoto wa kike nchini, Barrick ilikabidhi msaada wa kompyuta sita za kisasa 15 kwa ajili ya kuimarisha maabara ya kompyuta ya shule hiyo na kuwezesha wanafunzi kupata elimu kwa njia ya teknolojia ya kisasa ya kidigitali.

Msaada huo ulipokewa kwa furaha na Wanafunzi,wazazi na Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Taasisi ya Joha Trust inayoendesha shule za Wasichana ya Barbro Johansson nchini, Profesa Anna Tibaijuka, ambaye alishukuru jitihada ambazo zimekuwa zikifanywa na kampuni ya Barrick na Twiga kuunga mkono jitihada za kuboresha sekta ya elimu nchini ambapo alitoa wito kwa wazazi wa Tanzania na taasisi mbalimbali kuwekeza katika elimu ya watoto ili kuwaandaa watoto wa kitanzania kuwa wataalamu na kuhimili mabadiliko mbalimbali yanayoendelea kutokea kwa haraka siku hadi siku duniani.

Safari ya mtoto wa kike ina changamoto nyingi lakini kwa muongozo ufaao wasichana watafanikiwa hata hivyo wasichana wanasisitizwa kujiamini na kuamini ndoto zao na kuthubutu kutafuta ushauri na mwongozo kutoka kwa wale ambao wamefanikiwa kusafiri kwa njia moja.

Meneja Mawasiliano wa Barrick Georgia Mutagahywa, pia alisema Barrick itaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali na wadau mbalimbali katika kufanikisha vijana wa kitanzania wanapata elimu bora kwa kuwa inaamini elimu bora ni nyenzo kubwa ya kuleta maendeleo katika taifa.

“Msaada tulioutoa kwa shule hii na kwenye shule nyingine mbalimbali nchini ni kwa sababu ya imani yetu kubwa kwamba tukiwezeshwa mtoto wa kike atafanikiwa. Tunaamini katika uwezo wa wasichana na tunatekeleza jukumu letu katika kuwapa nafasi katika elimu bora kwa kuondoa vizuizi vingi kadiri tuwezavyo na kuwapa zana za kuwasaidia kuendelea katika elimu yao,” aliongeza.
Mkuu wa Shule hiyo Jospina Leonidas alishukuru kwa msaada huo na kueleza kuwa mafanikio ya shule hiyo yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku na kufanikisha ndoto ya kuwa shule bora ya wasichana nchini.

Post a Comment

0 Comments